
Serikali ya Tanzania na Zambia zimekubaliana kusitisha misaada kwa shirika reli Tanzania na Zambia kuanzia mwezi juni mwakani na kulitaka kupanga mikakati ya maendeleo itakayoliwezesha kujiendesha kibiashara.
Akizungumza katika halfa fupi ya kusaini makubaliano ya kupokea msaada wa vichwa vinne na mabehewa 18 yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 22.4, katibu mkuu wa wizara ya uchukuzi, Dkt Shaban Mwinjaka amelitaka shirika hilo kuanza kujianzaa kusimama lenyewe kuzalisha kupitia mipango ya maendeleo iliyowekwa na serikali za nchni mbili.
Kwa upande wake makamu wa rais wa shirika la wahandisi la China Bwana Zhao Zhongning amesema makabidhiano hayo ya mabehewa 18 na vichwa vinne yanaonyesha fursa mpya ya mipango ya Afrika ya kuunganisha Afrika katika karne ya 21 na kusisitiza shirika la wahandisi la China limeamua kujiiingiza sana katika maendeleoa ya reli ya Tazara kama sehemu ya kuwakumbuka wachina walipoteza maisha wakati wa ujenzi wa reli hiyo.
No comments:
Post a Comment