
Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limesema litachukua hatua kali za kisheria na kuwafukuza kazi askari wa jeshi wanaotuhumiwa kwa kula rusha kuwafanyia matendo ya kikatili kwa wananchi zuluma na kunyanyasa wananchi kwakuwa limesha choka kusikia malamiko hayo na wakati wa kuyafumbia macho umeshapita.
Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza na askari Polisi kutoka vitengo vyote na kutoa onyo huku akidai kuwa jeshi la Polisi linapaswa kufanya kazi kwa uadilifu na umakini mkubwa jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limeshacho kusikia malalamiko ya rushwa na uonevu kwa wananchi na sasa ni wakati wa kuchukua hatua.
Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Theopista Malya amesema baadhi ya askari wamekuwa wakilalamikiwa kwenda kinyume na taratibu na wengine wamekuwa wakiondoka katika vituo vya kazi kabla ya wakati huku mkuu wa upelelezi mkoa wa Arusha Muriro Jumanne akionya askari kuwa kuishi kwa kutegemea rushwa ni hatari na kwa kushirikiana na vitengo vingine wanahakikisha watakosha tabia hiyo.
No comments:
Post a Comment