Wednesday, January 28, 2015

Ufisadi mpya kutikisa Bunge

Ufisadi mpya kutikisa Bunge
Dar es Salaam. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kesho itawasha moto upya bungeni wakati itakaposoma ripoti maalumu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ikitarajiwa kuibua kashfa tatu nzito ikiwamo ya misamaha ya kodi.
Kashfa nyingine zinazotarajiwa kuibuliwa kesho ni, ufisadi katika gharama za ujenzi wa jengo la watu mashuhuri (VIP) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na uuzaji wa nyumba ya Bodi ya Korosho.

Sunday, January 25, 2015

Makinda: Siwatambui Chenge, Ngeleja

Makinda: Siwatambui Chenge, Ngeleja

SHARE BOOKMARKPRINTEMAILRATING

Spika wa Bunge, Anne Makinda akipokea kutoka kwa Balozi wa China hapa Nchini,  Dk LU Youquing baadhi ya vifaa vya Tehama vilivyotolewa na serikali ya China kwa ajili ya kusaidia shughuli za Bunge, katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi ya spika Dar es Salaam jana. Kulia ni Kamishna wa Bunge, Dk Maua Daftari. Picha na Venance Nestory 
Na Fidelis Butahe, Mwananchi

Posted  Alhamisi,Januari22  2015  saa 10:11 AM
KWA UFUPI
Kauli ya Makinda imekuja wakati akishukuru baada ya kupokea msaada wa vifaa mbalimbali vya mawasiliano na kazi kutoka Serikali ya China.
SHARE THIS STORY
 
 
 
0
Share
Dar es Salaam. Spika wa Bunge, Anne Makinda amesema hawatambui wenyeviti wa kamati tatu za kudumu za Bunge ambao Bunge liliazimia wavuliwe nyadhifa zao kutokana na kutajwa katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow.
Pamoja na kuwapo kwa maagizo ya Bunge, baadhi yao wanaendelea kujinasibu kuwa bado ni wenyeviti huku mmoja wao akiongoza vikao vya kamati.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Makinda alisema anachofahamu ni kuwa wenyeviti hao tayari wamaeshajiuzulu na kamati zao zinatakiwa kufanya uchaguzi wa wenyeviti wengine.
Wanaotakiwa kuachia nyadhifa zao ni Victor Mwabalaswa (Nishati na Madini), Andrew Chenge (Bajeti) na William Ngeleja (Katiba, Sheria na Utawala), ambaye hadi jana mchana alikuwa akiongoza kikao cha kamati hiyo.
Siku tano zilizopita Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah alieleza kuwa kamati hizo zinatakiwa kufanya uchaguzi na kwamba wenyeviti hao hawakutakiwa kuongoza vikao, lakini hadi jana, hakuna uchaguzi wowote uliokuwa umefanyika na baadhi wanaendelea na majukumu yao.
Katika mkutano wake wa 16 na 17, Bunge katika azimio lake la tatu, liliazimia kuwa watu walioshiriki katika kashfa ya miamala ya Akaunti ya Tegeta Escrow wakiwamo viongozi wa kamati hizo tatu, wachukuliwe hatua kabla ya kuanza kwa mkutano wa 18 wa Bunge unaotarajiwa kuanza Januari 27.
Ngeleja alikaririwa na gazeti hili hivi karibuni akisema kwamba anaendelea kushikilia nafasi hiyo kwa maelezo kuwa uchunguzi sakata hilo bado unaendelea na ikithibitika ndipo Bunge litachukua uamuzi ambao alisema atakuwa tayari kuutekeleza.
Bunge lapata msaada
Katika hatua nyingine, Makinda amesema Bunge litaanza kutumia vifaa teknolojia kuwasilisha taarifa mbalimbali na kuachana na utaratibu wa kudurufu nyaraka nyingi ili kuepusha gharama.
“Bunge linatumia zaidi ya Sh1 bilioni kudurufu miswada na nyaraka nyingine za wabunge. Sasa tunataka kutumia mfumo wa kisasa. Kila kitu kitakuwa katika kompyuta za wabunge,” alisema.
Kauli ya Makinda imekuja wakati akishukuru baada ya kupokea msaada wa vifaa mbalimbali vya mawasiliano na kazi kutoka Serikali ya China.
Balozi wa China nchini, Lu Youqing alimpatia Spika Makinda misaada ya vifaa hivyo vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) vyenye thamani ya Dola100,000.

Mwenyekiti auawa, viungo vyapikwa kama mboga

KITAIFA

Mwenyekiti auawa, viungo vyapikwa kama mboga

SHARE BOOKMARKPRINTEMAILRATING

Na Mussa Mwangoka 

Posted  Jumapili,Januari25  2015  saa 8:54 AM
KWA UFUPI
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari  mauaji hayo ya kikatili na  kutisha  yalitokea jana saa 5.30 usiku nyumbani kwa marehemu.
SHARE THIS STORY
 
 
 
0
Share
Mwenyekiti  wa Kitongoji    cha  Songambele, Kata ya Ilela Tarafa Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi, Richard Madirisha (31), ameuawa kikatili kwa kuchinjwa  shingo na kutenganishwa na kiwiliwili na kisha kunyofolewa  viungo vya mikono na miguu na sehemu za siri  na kichwa chake na viungo hivyo kupikwa ndani ya safuria kama mboga.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari  mauaji hayo ya kikatili na  kutisha  yalitokea jana saa 5.30 usiku nyumbani kwa marehemu.
Kidavashari alisema, siku hiyo ya tukio marehemu alikuwa amelala nyumbani kwake akiwa na mkewe  Meklina  Mussa na  ghafla walitokea watu watano ambao hawafahamiki na  kuvunja mlango na kuingia ndani ya nyumba.
Alisema watu hao waliodaiwa kuwa na mapanga  waliingia chumbani kwa marehemu  na kumlazisha mkewe ajifiche kwa kujifunika na shuka usoni.
 Alisema  baada ya mkewe kujifunika walianza kumchinja marehemu  kwa  kutumia panga huku mkewe akiwa anasikia jinsi marehemu  akilia kwa uchungu.
Kidavashari alisema baada ya kumchinja walichukua kichwa na kukiweka kwenye safuria na maji na kukipika kwenye moto uliokuwa unawake nje ya nyumba ya marehemu.
Alisema kisha walirudi ndani na kunyofoa sehemu za siri, mikono na miguu  na  kuziweka kwenye  safuria  jingine  kwenye moto   na kutokomea kusikojulikana huku  viungo hivyo vikiendelea kuchemka  ndani ya safuria hizo.
 Kidavashari alisema  mke  wa marehemu baada ya kuona watu hao wametokomea alitoka nje na kwenda kutoa taarifa kwa majirani ambao walifika kwenye eneo hilo  na kukuta viongo hivyo vikiwa  ninaendelea kuchemke  kwenye safuria hizo huku kiwailiwili chake kikiwa ndani ya chumba chake

 Amesema uchunguzi wa  awali umebaini kuwa chanzo cha mauwaji  kimetokana na visa vya marehemu na mtu mmoja ambae walikuwa wakiishi nae Tabora  ambae  alikuwa akimtuhumu marehemu  kuwa amemnyanya  mwanamke ambae walikuwa  na mahusiano nae ya kimapenzi ambae marehemu aliamua   kuhama nae kijijini  hapo na kuhamia nae kijiji cha Songambele  Wilaya Mlele

 Kamanda Kidavashari  alieleza   jeshi la polisi Mkoa wa Katavi limewakamata na linawashikilia  watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauwaji hayo ya kikatili

hahahahaha simbaaaa mmetoka suruu na azamu duuuuuuu

Leo ndio leo uwanja wa taifa wakati wekundu wa Msimbazi Simba watakapowakaribisha mabingwa watetezi Azam FC katika mchezo wa ligi kuu.
Nini utabiri wako?

filamu mpya ya nani mtamu iko sokoni nw


kaa tayari kupata kazi mpya inayokwenada  kwa jina la nani mtamu 
 nifilamu ya  kibongo inatoka ivi karibu ikisambazwa na wasambazaji wako  wa hap hapa inchini 

Friday, January 23, 2015

huyu ndiyo  mjasiliamali aliotusua hapa 
tanzania kwa uuzaji wa miguu ya kuku 

Monday, January 5, 2015

PICHA ZA UCHI ZA MAMA WEMA SEPETU ZASAMBAZWAA...WEMA ALIPOZIONA AZIMIA

PICHA ZA UCHI ZA MAMA WEMA SEPETU ZASAMBAZWAA...WEMA ALIPOZIONA AZIMIA

Posted by joni fide at 3:11 AM 0 Comments



Diva katika tasnia ya filamu Bongo Wema Isaac Sepetu 'Beautiful Onyinye'.

Katika jambo ambalo limeuumiza moyo wa Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu 'Beautiful Onyinye' tangu awe staa, ni ishu iliyotokea wikiendi iliyopita baada ya mtu asiyejulikana kutengeneza picha chafu ya mama mzazi wa mrembo huyo, Mariam Sepetu na kisha kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii kitu ambacho kilimshtusha na kujikuta akipoteza fahamu 
Akizungumza mmoja wa marafiki zake wa karibu ambaye aliomba chondechonde asitajwe , mara ya mwisho kuona chozi la Wema ni siku ya msiba wa marehemu baba yake, mzee Isaac Sepetu lakini hili lilizidi kilio kile kwani ni tukio la udhalilishaji kwa mzazi wake huyo hivyo kuzimia ilikuwa ni lazima kwani yaliyomkuta yanasikitisha.
Chanzo hicho kilidai kwamba, Wema hakutegemea kama ipo siku mama yake atadhalilishwa kiasi hicho hadi kufikia yeye kupoteza fahamu.
"Kiukweli ile picha ilichafua sana hali ya hewa hasa kwa wanaompenda Wema na hata kwa wanaomchukia Wema kwani kila mmoja alikuwa analaani kitendo kile ambacho si cha kiungwana.
"Unajua inafika hatua unatakiwa ufahamu mama wa mwenzio ni mama yako pia halafu usifurahie ubaya anaofanyiwa mama wa mwenzio tutukanane sisi wenyewe na si kuwaingiza wazazi kwenye mambo wasiyojua mbele wala nyuma," kilidai chanzo hicho.
"Hebu fikiria mama yako mzazi atengenezewe picha ya utupu na jamii iaminishwe kuwa ni yeye wakati si kweli, inauma sana jamani. Utadhani huyo mtu hajazaliwa na mama."
TIMU DENGUE NA MKAKATI MZITO
Katika kipindi cha vuguvugu la kuchafuana kilichoanza mwanzoni mwa wiki iliyopita, kuna wachangiaji katika mitandao ya kijamii waliojiita kwa jina la Timu Dengue, walionekana kumkandia Wema.
Chanzo chetu kinadai kuwa, timu hiyo ina mkakati mzito wa kumchafua Wema kwa kila namna.
"Wamepanga mkakati mzito, wanadai eti Wema anajisikia. Lakini watu wanasema haiwezekani watu wafanye mambo bila sababu. Sasa hapo wanamhusisha Kajala (Masanja) kwa kuwa ndiye mtu aliye na bifu naye kwa sasa," kilipasha chanzo hicho na kuongeza:
"Lakini kuna wengine wanabishana, wanadai kuwa inawezekana watu wasio na kazi za kufanya au wenye chuki binafsi na Wema wameamua kutumia mwanya huo kumchafua Wema na familia yake wakiamini lazima Kajala atahusishwa kwa kuwa ana ugomvi naye."
BOFYA HAPA KUMSIKIA WEMA
Tulipoishuhudia picha hiyo ya utupu na kujiridhisha kuwa siyo ya mama Wema, tulimtafuta Wema kuzungumzia ni kwa jinsi gani alivyoumia baada ya kuona picha ile ambapo majibu yake alionekana bado ana maumivu makali ambayo yalidhihirisha wazi yalikuwa  hayajamuisha moyoni.
"Nimeumia sana mama yangu kudhalilishwa na si mimi tu familia yangu yote kwa jumla, tumeumizwa sana kwa tukio lile lakini mimi nasema namuachia Mungu kwani yeye ndiye anajua ila siyo siri ni tukio ambalo lilinifanya niugue ghafla," alisema Wema na kuongeza:
"Yaani nilikuwa napewa pole nyingi sana utadhani mimi mgonjwa. Hata wale ambao hawanipendi nao walikuwa wakinipa pole. Naomba serikali itazame upya hili suala hili la watu kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii."
e: medium;">AUNT EZEKIEL AFANYA KAZI YA ZIADA
Katika ishu hiyo, staa mwenzake wa sinema za Kibongo ambaye kwa sasa ni mashosti, Aunt Ezekiel Grayson alifanya kazi ya ziada kumuokoa Wema na kumfariji asichukue uamuzi mgumu.
Inaelezwa kuwa, Aunt alitumia dakika 29 kumpepea shosti wake huyo ili aweze kurejewa na fahamu, jambo zoezi ambalo lilizaa matunda.
Akizungumza Aunt alisema tukio hilo limemuumiza kila mtu hata wale ambao wanaonekana wako tofauti na Wema lakini kwa hili nao wameumia na kuungana naye kumtetea na kuwakemea waliyofanya kitendo kile.
Mama Wema.
"Nimeumia kwa tukio ambalo limefanywa na kusababisha Wema wangu kulia sana hadi kufikia kuumwa ghafla na kupoteza fahamu. Dah! Binadamu wengine sijui tukoje, lakini hamtaweza kufanikisha kwa sababu Wema ana watu wengi wanaompenda kuliko wanaomchukia," alisema Aunt.
KAJALA SASA
Tulimtafuta Kajala kupitia simu yake ya mkononi ili kujibu tuhuma za  kuhusishwa na picha hiyo lakini simu yake ilikuwa ikikatika kila ilipopigwa.
Baadaye ilijulikana kuwa, aliamua kuifunga kwa muda (inawezekana alikuwa sehemu inayohitaji utulivu).
Baadaye akatumiwa ujumbe uliosomeka: "Habari. Una taarifa ya picha chafu ya kutengenezwa ya mama Wema iliyosambazwa mitandaoni? Lakini unatajwa kuhusika kwa sababu una bifu na Wema, unasemaje?"
 Kajala hakujibu meseji hiyo wala kupiga simu 
MAMA WEMA ANASEMAJE?
Jitihada za kuzungumza na mama Wema juu ya sakata hilo ziligonga mwamba kwani simu yake iliita bila kupokelewa.
Msanii Kajala Masanja aliyetajwa katika sakata hilo.
SERIKALI NAYO
Timu yetu ilijaribu kufanya mawasiliano na Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba bila mafanikio, kwani simu yake haikupatikana.
Hata hivyo, wananchi wametoa kilio chao kwa Wizara ya Sayansi na Teknolojia kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kudhibiti usambazwaji wa picha chafu mitandaoni.
TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni, kuliibuka picha chafu katika mitandao ya kijamii za waheshimiwa wabunge, kabla ya baadaye wabunge kulaan ambazo mpaka sasa hazijulikana kuwa zilikuwa halisi au za kutengen
TAHADHARI
Kumekuwa na wingu la kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii ambapo ukiacha watu maarufu kutengenezewa picha chafu pia wanafunzi wa vyuo wamekuwa waathirika wakubwa hivyo ni vyema kila mtu akachukua taadhari na mamlaka husika ilishughulikie.
Tags: 
Share This Post
Get Updates
Subscribe to our Mailing List. We'll never share your Email address.


0 MAONI:


Total Pageviews

56869

Yyyy


Powered by Blogger.
back to top


PESA YAIMBA WIMBO