Tuesday, February 10, 2015

Wanafunzi walionusurika na moto shule ya sekondari ya Idodi warudishwa nyumbani mkoani Iringa.

Wanafunzi walionusurika na moto shule ya sekondari ya Idodi warudishwa nyumbani mkoani Iringa.
Uongozi wa mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na bodi ya shule ya sekondari ya Idodi mkoani humo wamewarudisha nyumbani watoto 190 wa kidato cha pili na cha nne ambao bweni lao lilishika moto na kuungua hapo jana na kuteketeza vifaa vyao vyote ili kupisha maandalizi ya kutafuata mahali pakuwahifadhi kwa muda wakati ufumbuzi wa kudumu wa tatizo lao ukiendelea.
Moto huo uliozuka majira ya saa nne na nusu asubuhi wakati wanafunzi wakiwa darasani uliteketeza bweni hilo linalokaliwa na wasichana wa kidato cha pili na cha nne shuleni hapo na kuwaacha wanafunzi hao wanaojiandaa na mitihani ya kidato cha pili na ule wa kumaliza kidato cha nne wakiwa hawana pakulala lakini zaidi hata vifaa yakiwemo madaftari yaliyojaa notes zao nayo yameteketea.
 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza ameuagiza uongozi na bodi ya shule hiyo kumleta mtaalam wa mfumo wa umeme ili aweze kukagua mfumo wa umeme wa shule hiyo huku mwenyekiti wa bodi akieleza kuwa kutokana na tukio hilo wameamua pamoja na mambo mengine kuwaondoa shuleni hapo wanafunzi 192 waliounguliwa na vifaa vyao pamoja na kuwahamisha kwa muda wale wengine ambao bweni lao lilinusurika na moto huo lakini vifaa vyao vingi vikiharibika wakati wa zoezi la uokoaji.
 
Hii ni mara ya pili kwa bweni la wasichana kuteketea kwa moto katika shule ya sekondari Idodi ndani ya kipindi cha miaka mitano ambapo mwaka 2009 bweni lingine la wasichana katika shule hiyohiyo liliungua moto usiku wa manane na kuteketeza wasichana 12 waliokuwa wamelala kwenye bweni hilo kiasi cha kutotambulika.
 

Taasisi ya kuzuia na kupamba na rushwa

Taasisi ya kuzuia na kupamba na rushwa -Takukuru imembadilishia hati ya mashtaka ya mkurugenzi wa huduma za sheria wa wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Rugonzibwa Mujunangoma aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kupokea rushwa ya sh 323 milioni toka kwa James Rugemalira na kuondolewa maneno kuwa fedha hizo ni sehemu ya akaunti ya Tegeta Escrow.

Moto mkubwa umeteketeza ghorofa ya pili ya jengo la Consolidated Investment Tanzania Limited jijini Dar es Salaam.

Moto mkubwa umeteketeza ghorofa ya pili ya jengo la Consolidated Investment Tanzania Limited jijini Dar es Salaam.
Moto mkubwa umeteketeza kabisa ghorofa ya pili ya jengo la Consolidated Investment Tanzania Limited huku baadhi ya familia zinazoishi katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo wakiwemo watoto wakinusurika baada ya kuokokolewa na jeshi la polisi jijini Dar es Salaam.
Moto huo mkubwa ambao chanzo chake hakikufahamika mara moja umeteketeza kabisa ghorofa ya pili ya jengo hilo la Consolidated Investment Tanzania Limited lililopo katika mtaa wa Libya na msikiti Kisutu jijini Dar es Salaam huku mashuhuda wa moto huo wakionekana wakiwa makini kupiga picha katika simu zao pengine kutokana na kukuwa kwa teknolojia.
 
Jeshi la polisi lilifika mapema katika eneo la tukio wakiongozwa na kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova kwa nia ya kuimarisha ulinzi na kuzuia tabia iliyozoeleka ya baadhi ya wakazi wa jiji kutumia majanga ya moto na ajali kama fursa ya kujipatia chochote ambapo mashuhuda wamelizungumzia tukio hilo.
 
Akizungumza mara baada ya moto huo kuzima kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam amewaambia waandishi wa habari kuwa upelelezi wa kitaalam, juu ya chanzo cha moto huo bado unaendelea na kuongeza kuwa kwa kiasi kikubwa jeshi hilo limefanikiwa kudhibiti vitendo vya kihalifu kufanyika katika tukio hilo pamoja na kufanya uokozi.
 
Jicho la tatu la ITV likashuhudia namna zimamoto walivyokuwa wakihaha kupata maji ya kutosha ya kuuzima moto huo kabla ya kuongezewa nguvu na vikosi vya zimamoto na uokoaji kutoka bandari na uwanja wa ndege wakati katika majengo jirani kukiwa na matanki lukuki yenye maji yaliyokuwa yakimwagika bila ya matumizi jambo lililochangia kwa kiasi kikubwa jengo hilo kuendelea kuteketea licha ya uwepo wa maji hayo karibu kabisa ambayo endapo yangetumika huenda madhara katika ghoro hiyo ya pili yasingekuwa makubwa kiasi hiki jambo ambalo kamishna wa kikosi cha ukoaji na zimamoto analizungumzia.
 

Monday, February 9, 2015

Unaambiwa Penzi La Wema Sepetu na Ommy Dimpoz si Siri Tena, Wapiga Picha Wakiwa Bafuni , Wema Ndani ya Taulo

Unaambiwa Penzi La Wema Sepetu na Ommy Dimpoz si Siri Tena, Wapiga Picha Wakiwa Bafuni , Wema Ndani ya Taulo

Ule usema unaosema Lisemwalo lipo hatimae umekaribia kutimia , Baada jana kuwawekea picha hapa ya Wema Sepetu na Ommy Dimpoz Wakikamuana Chunusi na watu wengi kutoa maoni kusema kuwa kuna kitu kinaendelea kati yao....

Wenyewe kwa kudhihirisha hilo usiku wa jana wamepost picha wakiwa pamoja bafuni huku wema akiwa ndani ya taulo jeupe na Ommy Dimpoz akinawa mikono kwenye Sinki ..Hii ni ushahidi tosha kwambo asilimia karibia 90 kuna kitu kinaendelea kati yao....

Ben Paul Amerudi Tena Katika Masikio yako, Wimbo wake Mpya Huu Hapa

Ben Paul Amerudi Tena Katika Masikio yako, Wimbo wake Mpya Huu Hapa

Baada ya Kukaa Muda Mrefu Bila Kutoa Wimbo Mpya Udaku Specially Inakupa nafasi ya kusikiliza Wimbo Mpya wa kutoka kwa Mwanamuziki Ben Pol Kipenzi cha Mabinti Unaitwa Sophia , Umetengenezwa na kufanyiwa mixing na Producer Swaki ...

Dawa ya Mapenzi, Mvuto, Kumvuta Aliyembali, Kumshika Mpenzi Yapigwa Marufuku

Dawa ya Mapenzi, Mvuto, Kumvuta Aliyembali, Kumshika Mpenzi Yapigwa Marufuku

Kumekuwa na tabia hasa kwa wanawake kwenda kwa waganga na kutaka dawa na kumvuta mpenzi ama kumdhibiti mwaname
Sasa kwa taarifa yako kwa wale wanaopenda kutumia Ushirikina kwenye suala la Mapenzi sasa mwisho wao umewadia, Serikali imeshapiga marufuku Waganga wa kienyeji wenye shughuli zinazohusiana na kupiga ramli.

Jipangeni upya mapenzi si ramli wala Mitishamba..
Huko kwa waganga mnaenda kudanganywa tu na mwisho kujikuta kutumia hela nyingi sana bila sababu , na kuna habari kuwa waganga wengine wanakulala kwanza wewe wakidai wanakuwekea dawa kwa njia ya kufanya mapenzi ili uwe na mvuta kama inavyoonekana hapo kwenye picha..

Akila Kimkichwa mapenzi si Ndumba Jamani

Dawa ya Mapenzi, Mvuto, Kumvuta Aliyembali, Kumshika Mpenzi Yapigwa Marufuku

Kumekuwa na tabia hasa kwa wanawake kwenda kwa waganga na kutaka dawa na kumvuta mpenzi ama kumdhibiti mwaname
Sasa kwa taarifa yako kwa wale wanaopenda kutumia Ushirikina kwenye suala la Mapenzi sasa mwisho wao umewadia, Serikali imeshapiga marufuku Waganga wa kienyeji wenye shughuli zinazohusiana na kupiga ramli.

Jipangeni upya mapenzi si ramli wala Mitishamba..
Huko kwa waganga mnaenda kudanganywa tu na mwisho kujikuta kutumia hela nyingi sana bila sababu , na kuna habari kuwa waganga wengine wanakulala kwanza wewe wakidai wanakuwekea dawa kwa njia ya kufanya mapenzi ili uwe na mvuta kama inavyoonekana hapo kwenye picha..

Akila Kimkichwa mapenzi si Ndumba Jamani

Mike Mushi wa Mmoja wa Waasisi wa JamiiForums kwenye kipindi cha MKASI

Mike Mushi wa Mmoja wa Waasisi wa JamiiForums kwenye kipindi cha MKASI

Katika ulimwengu huu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, fursa nyingi zimejitokeza katika jamii yetu! Moja ni uharaka wa kusambaa kwa habari, njema au mbaya; upatikanaji wa jukwaa la watu kutoa maoni yao....lakini la zaidi....imefungua nafasi lukuki za vijana kujiajiri na kuajiri mamia kama sio maelfu ya wengine..

Mfano hai hapa Tanzania ni Jamii Forum! Wengi tunaufahamu kwa umahiri wake wa mijadala mbali mbali na zaidi ya kisiasa, ukiwa kama mtandao wa kwanza wa jamii wenye mizizi yake Tanzania kupata kukubalika na watu wenye hulka tofauti. Kitu ambacho wengi wetu hatujui ni.....Ni Nani Alie Nyuma ya Injini za JamiiForums?

Leo tunawaletea mmoja wa vinara wanaoiweka JF hewani na kutupa sisi uwezo kujinafasi, Mjasiriamali Kijana, Mtanashati na Mwenye akili za Kipekee.....Bw. Mike Mushi!

‪#‎MikeMushi‬ ni nani? Katokes wapi? Nini ndoto zake? Tutegemee nini kutoka kwake na timu yake siku za karibuni? Na nini nafasi ya JF katika harakati za uchaguzi na maamuzi ya katiba mwaka 2015?

Jiunge nasi saa 3:30 usiku, EATV, kwani Salama, Mubah na John....hawataacha kigae bila kukipindua!

Source: MkasiTV

Uongozi wa Msanii Chris Brown Upo Tayari Kufanya Kazi na Ally Kiba

Uongozi wa Msanii Chris Brown Upo Tayari Kufanya Kazi na Ally Kiba

Uongozi wa muziki nchini marekani unao muongoza msanii wa R&B Chris Brown umetoa taarifa kwa uongozi wa muziki Tanzania unao muongoza msanii kutoka Tanzania ALI KIBA msanii ambae yupo chini ya uongozi wa Kampuni za SAMSUNG....

Zimamoto wajitetea ajali ya moto Dar

KITAIFA

Zimamoto wajitetea ajali ya moto Dar


Gari la zimamoto 
Na Laura Paul, Mwananchi

Posted  Jumatatu,Februari9  2015  saa 17:26 PM
KWA UFUPI
Katika tukio hilo, Emmanuel Mpira ambaye ni mtoto katika familia hiyo ndiye aliyenusurika kwani alikuwa matembezini ambapo aliporudi alikuta moto umeshaanza kuwaka na baadhi ya vitu vilishaanza kuteketea.

 
 


Dar es salaam, Siku tatu baada ya ajali ya moto kutokea  katika eneo la Kipunguni A jijini Dar es Salaam na kusababisha vifo vya watu sita na nyumba kuteketeatu, Jeshi la Zimamoto limejitete kuwa lilishindwa kufika haraka kwenye tukio kwa sababu ya ubovu wa mawasiliano kati yao na wananchi.
Katika tukio hilo, Emmanuel Mpira ambaye ni mtoto katika familia hiyo ndiye aliyenusurika kwani alikuwa matembezini ambapo aliporudi alikuta moto umeshaanza kuwaka na baadhi ya vitu vilishaanza kuteketea.
Inspekta wa Jeshi la Zimamoto, Puyo Nzalayaimis ameeleza kuwa wananchi wasiwalaumu kwa sababu taarifa zilichelewa kufika ofisini kwao na kuongeza kuwa mawasiliano yalikuwa mabovu.
Amesema alipokuwa anatoka kuelekea eneo la tukio walipotea njia na kuelekea hadi Kituo cha Polisi cha Sitaki Shari na badae wasamaria wema waliwaelekeza hadi eneo la tukio.
“Katika nyumba hiyo hakikuwezwa kuokolewa hata kitu kimoja kwasababu vitu vyote vilishaanza kushika moto na zima moto walipofika eneo la tukio waliweza kumalizia kuuzima na kutoa miili ya marehemu na kukabidhi kwa Jeshi la Polisi,”amesema Nzalayaimisi
Ameongezea kwa sasa jeshi hilo linakabiliwa na changamoto nyingi  ikiwemo uhaba wa  magari  , mawasiliano mabovu na kutojua mitaa mingi ya jijini Dar es Salaam.
Aliwashauri wananchi kutoa taarifa kamili na watu wanapojenga nyumba wahakikishe wanakuwa na milango na madirisha  ya dharula.

Vita ya Mrema, Mbatia sasa mot

KITAIFA

Vita ya Mrema, Mbatia sasa moto

SHARE BOOKMARKPRINTEMAILRATING
Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbati akimweleza jambo Mbunge wa Vunjo, Augustino Mrema walipohudhuria kikao cha Bunge, mjini Dodoma jana. Mrema alitoa maelezo yake binafsi bungeni juzi, akimtuhumu Mbatia kumchafua jimboni kwake. Picha na Edwin Mjwahuzi      
Na Fidelis Butahe na Sharon Sauwa, Mwananchi

Posted  Februari7  2015  saa 9:35 AM
KWA UFUPI
Ni vita ya kuwania ubunge wa Jimbo la Vunjo katika Uchaguzi Mkuu ujao.

 
 


Dar/Dodoma. Vita ya ubunge baina ya wenyeviti wawili wa vyama vya upinzani, James Mbatia na Augustine Mrema imezidi kupamba moto baada ya kushambuliana bungeni kuhusu kusigana kwenye harakati za ubunge wa Jimbo la Vunjo.
Kwenye vikao vya Bunge na nje, Mrema, mwenyekiti wa TLP, amekuwa akimlalamikia Mbatia (NCCR-Mageuzi) kuwa anamuingilia kwenye jimbo lake, lakini juzi alikwenda mbali zaidi alipoomba kuwasilisha taarifa ya hali yake kiafya na kutumia nafasi hiyo kumshambulia mpinzani wake, ambaye pia jana aliomba nafasi kama hiyo kujibu mapigo.
Msuguano wa wawili hao, ambao waliwahi kuwa pamoja kwenye Chama cha NCCR, ulitokana na uamuzi wa Mbatia kutangaza nia ya kugombea ubunge wa Vunjo, jimbo ambalo kwa vipindi viwili limekuwa chini ya Mrema.
Juzi usiku, Mrema, ambaye pia amewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Temeke, alisoma taarifa hiyo ya hali yake ya afya akisema kuwa yeye si mgonjwa kama inavyodaiwa na atagombea tena ubunge kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Katika taarifa yake aliyoimbatanisha na ripoti za madaktari kuhusu vipimo alivyofanya na ambayo alitumia dakika 15 kuisoma, Mrema alimtuhumu Mbatia kwamba amevamia jimbo hilo na kuwambia watu wasiwachague wagombea wa TLP, akiwamo na yeye (Mrema) kwa sababu ni marehemu mtarajiwa, ana saratani na Virusi vya Ukimwi.
Akieleza jinsi Rais Jakaya Kikwete na Spika Anne Makinda walivyofanikisha safari zake za kwenda nchini India, kuchunguzwa afya yake, kutibiwa saratani ya mapafu pamoja na kupima Ukimwi, Mrema alisema: “Awali nilikuwa na saratani ya mapafu, lakini baada ya kupata matibabu kwa mwaka mmoja, nimepima tena na ripoti za madaktari zinaonyesha kuwa nimepona.
“Nilipima na ukimwi na vipimo vimeonyesha sina maambukizi yoyote. Kweli Mungu mkubwa. Hafi mtu hapa. Mimi ni mzima wa afya na nitagombea ubunge maana ndiyo unanitoa roho.”
Hata hivyo, Mbatia, ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na Rais, jana jioni alikanusha madai hayo bungeni akisema hayana ukweli wowote.
“Sijawahi kumnyanyapaa mtu mwenye Ukimwi. Kuzeeka hakuna mjadala ila kuwa na busara ni uamuzi tu. Hakuna mwenye hati miliki ya uongozi, wenye hati miliki ni wananchi,” alisema.
Mbatia alitangaza nia hiyo ya kugombea ubunge wa Vunjo Julai 29, mwaka jana, ikiwa ni siku moja baada ya wafuasi wa vyama vya CCM, Chadema, NCCR-Mageuzi na TLP kumwita jimboni humo, wakimtaka achukue uamuzi mgumu ya kurejea nyumbani kugombea ubunge. Mbatia amewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo mwaka 1995 hadi 2000.
Akifafanua madai yake juzi, Mrema alidai Desemba mwaka jana akiwa katika matibabu India, Mbatia na wapambe wake ambao ‘wamepiga kambi’ katika jimbo hilo, walitumia mwanya huo kufanya mikutano ya hadhara waliyoipa jina la Delete TLP (futa TLP), kuwaeleza wananchi kuwa yeye (Mrema) ni marehemu mtarajiwa, hivyo hatakiwi kuchaguliwa kuwa mbunge.
“Waliwashawishi wananchi kutochagua wagombea wa TLP katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vitongoji kwa sababu ya afya yangu. Mbatia anataka yeye ndiyo achaguliwe kwa kuwa ana afya nzuri,” alisisitiza. Mrema alisema muda wa kampeni haujafika na wala jimbo la Vunjo halijatangazwa na serikali kuwa lipo wazi, hivyo kitendo cha Mbatia kuanza kampeni mapema ni kinyume na Sheria ya Uchaguzi.


Madabida: Sina kambi, wanaohangaika hawajielewi

Madabida: Sina kambi, wanaohangaika hawajielewi



Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madai

Posted  Jumatatu,Februari9  2015  saa 17:42 PM
KWA UFUPI
Madabida aliitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki, wakati alipokuwa akitoa shukrani kwa  wananchi wa Mtaa wa Kijichi  kwa kukipa kura chama cha Mapinduzi katika uchaguzi wa serikali za Mitaa, kijiji na kitongoji 2014.

 
  
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida amesema yeye hayumo kwenye  kambi yoyote ya  wanaharakati wanaowania urais ndani ya CCM na kusisitiza kuwa   kambi yake ni moja tu CCM.Madabida aliitoa kauli hiyo wakatialipokuwa akitoa shukrani kwa  wananchi wa Mtaa wa Kijichi  kwa kukipa kura chama cha Mapinduzi katika uchaguzi wa serikali za Mitaa, kijiji na kitongoji 2014.
“Madai hayo siyo ya kweli, mimi sipo katika kambi yoyote,  kambi yangu moja tu Chama cha Mapinduzi.” Madabida ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuwashukuru wananchi hao wa mtaa wa kijichi kwa kukipa kula chama cha CCM kwa niaba ya Mwenyekiti wa mtaa huo, Ramadhan Kiula. 
Akizungumza na wananchi hao, Madabida alisema nchi yetu inachangamoto nyingi ikiwamo za kiuchumi, kisiasa na kijamii  na kwamba CCM inajitahidi kukabiliana nazo  hivyo aliwataka wananchi wasifanye wasifanye makosa katika uchaguzi ujao kwa sababu  sumu haionjwi.
Madabida amesema kuhusu Katiba  inayopendekezwa  mengi  yamesemwa na yanaendelea kusemwa lakini ni kweli ajenda yake ni ya CCM ambayo ipo madarakani, siyo ya wapinzani  ila Katiba siyo ya CCM ni ya wananchi.
“Rasimu ya pili ya  Katiba haikuwa Msahafu ama Biblia, ndiyo maanda kulikuwepo na bunge maalum la Katiba ambapo lengo lilikuwa ni kuijadili, kuichambua na inapobidi kubadilishwa na lilifanya hivyo  kwa kufanya mabadiliko ya maboresho katika mambo mapya kwa asilimia 15 kati ya 100.”Alisema Madabida.
Kuhusu uchaguzi wa uchaguzi wa serikali za Mitaa, kijiji na kitongoji 2014, Madabida alikiri kuwa kulikuwepo na ushindani mkubwa  na akaongeza kuwa kuna  mambo mengi wamejifunza  ambayo yatatusaidia  katika uchaguzi ujao.
Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk Faustine Ngugulile aliwataka wananchi hao kuisoma katika inayopendekezwa kwa kina na katiba ya zamani ili waweze kufahamu wanapiga kura ya nini.
Dk Ndugulile alisema wao kama CCM wanasema Katiba hiyo inayopendekezwa inatosha na kuwataka wananchi wasije kurubuniwa  ifikapo Aprili 30,2015 wajitokeze kuipigia kura.
Pia aliwataka wananchi kujitokeza katika kujiandikisha kwa kuwa wasipofanya hivyo kula ya maoni n ahata uchaguzi mkuu hawatashiriki kwa sababu vitambulisho vya vya zamani vitakuwa havina tena thamani.

Baba mkubwa aliyetajwa kwa jina la Mohamed Said a.k.a Muddy

Baba mkubwa aliyetajwa kwa jina la Mohamed Said a.k.a Muddy, mkazi wa Tegeta-Msufini jijini Dar amepigwa pingu akituhumiwa kumfanyia ukatili wa kutisha wa kumsulubu mtoto wa kiume wa mdogo wake, mwenye umri wa miaka 6( jina linahifadhiwa). Inadaiwa kuwa Muddy alimchukua mtoto huyo kutoka kwa wazazi wake wanaoishi mkoani Mtwara kwa lengo la kuja naye Dar kwa ajili ya kumsomesha lakini kinyume na lengo hilo, jamaa huyo alipomfikisha Dar ilidaiwa alianza kumfanyia ukatili mtoto huyo wa dozi ya vipigo. Majirani walisema kuwa jamaa huyo amekuwa akimshushia kipigo mtoto huyo mara kwa mara kwa kutumia bomba la plastiki na waya wa umeme huku adhabu kama kumnyanyua miguu juu kichwa chini, kumnyanyua juu kwa kumshika masikio na kushinda muda mrefu bila kula vikiwa ni sehemu ya maisha ya mtoto huyo.
Una lipi la kusema juu ya tukio kama hili?

amefariki dunia

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi... huyu ndie mama mashaka wa kaole sanaa group.. tuko msibani tunajiandaa kwenda Mzinga kuzika... pia alishawahi kufanya tangazo la foma la mtaa nzasa...
Like ·  · 

PESA YAIMBA WIMBO