
Maafisa wa TRA wamelazimika kufanya ukaguzi wa awali katika makontena tisa yaliyokamatwa katika eneo la Mbezi Tanki Bovu jijini Dar es Salaam ili kujidhihirisha iwapo makontena hayo yalilipiwa kodi au lah.
Katika kufuatilia sakata hilo, ITV ililazimika kufika katika eneo hilo kwa mara nyingine tena majira ya usiku na kukuta maafisa wa tra wakiwa tayari katika eneo hilo kufanya ukaguzi wa awali katika makontena hayo na kubaini kwamba yaliingizwa nchini kutoka nchini China na kwamba zilitolewa bandari bila kukwepa kodi kama ilivyokuwa ikidhaniwa.
Baadhi ya wahusika waliokuwa wakihusika kusafirisha makontena hayo ambao ni PMM ICD wamesema walilazimika kuleta makontena katika eneo hilo ili kuyahifadhi kabla ya kumfikishia mteja wao na si kwamba wamefanya hivyo kwa kukwepa kodi ya aina yeyote huku mmiliki wa Heritage Empire co LTD mbali na kueleza kuwa mali hiyo haina mashaka kwani ilimeingizwa nchini na kuondolewa katika eneo la bandari kwa kufuata taratibu zote lakini alishikwa butwaa baada ya kuona mali makontena yake yamefikishwa katika eneo la Mbezi na si eneo la uwekezaji Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment