Sunday, December 6, 2015

Maafisa 39 wa Magereza hapa nchini wakabidhiwa bendera ya Taifa kupeperusha siku ya maadhimisho ya uhuru.

Maafisa 39 wa jeshi la Magereza nchini wamekabidhiwa Bendera kwa ajili ya kuanza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Uhuru pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani.
Akikabidhi bendera hiyo kwa maafisa kutoka Magereza nane  hapa nchini mkuu wa Jeshi la Magereza nchini kamishna CASMIR.John Minja amesema bado tatizo la msongamano wa wahalifu katika magereza ni kubwa.
 
Amesema uwezo wa magereza hapa nchini ni kuhifadhi wafungwa 25000 lakini kwa sasa wanahifadhi wafungwa na mahabusu 34,000 na kwamba tatizo kuibwa liko katika maeneo ya miji mikubwa.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya utalii klabu jeshi la Magereza hapa nchini Bw.Estomii Hamis amewashihi watanzania kujenga tabia ya kutembelea vivutio vya utalii hususani kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka kuliko kuachia watalii kutoka nje ya nchi.
 
Nao baadhi ya maafisa hao wanaopanda mlima Kilimanjaro wamesema umefika wakati sasa kwa watanzania kuthamini vivutio vilivyopo hapa nchini na kwamba mbali  na kujionea vivutio mbalimbali pia nchi itajipatia mapato.
 

No comments:

Post a Comment

PESA YAIMBA WIMBO