Wednesday, December 9, 2015

‪#‎Habari‬ Mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) kwa kushirikiana na jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani mkoani Dodoma wamefanya ukaguzi wa kushtukiza kwenye

‪#‎Habari‬ Mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) kwa kushirikiana na jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani mkoani Dodoma wamefanya ukaguzi wa kushtukiza kwenye kituo kikuu cha mabasi mkoani humo na kubaini baadhi ya mabasi kutokidhi usalama wa usafirishaji abiria huku mengine yakitoza nauli maradufu kinyume na bei elekezi iliyotolewa na mamlaka hiyo.
Katika ukaguzi huo ulioanza mapema alfajiri kwenye kituo kikuu cha mabasi yanayosafiri kutoka Dodoma kwenda mikoa mbalimbali na nchi jirani maofisa wa SUMATRA na jeshi la Polisi pia wakatumia fursa hiyo kutoa elimu kwa abiria juu ya usalama wao wawapo safarini ikiwa ni pamoja na kuripoti mara moja mienendo mibaya ya madereva katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka ambacho wasafiri wanaongezeka.

No comments:

Post a Comment

PESA YAIMBA WIMBO