Wednesday, December 9, 2015

Zoezi la Polisi kupambana na ugaidi lazua taharuki kwa wananchi bariadi mkoani Simiyu.

Wananchi wa mji wa Bariadi mkoani Simiyu husuan wafanyabiashara wa maduka wameshikwa na taharuki kubwa kufatia zoezi la kupambana na magaidi lililofanywa na askari polisi wa mkoa huo.
Zoezi hilo ambalo limefanyika eneo la soko kuu majira ya saa tano limezuia taharuki huku wananchi wakianguka hovyo wakidhani wamevamiwa na majambazi baada ya watu waliovalia nguo nyeusi kuvamia eneo hilo na kufyatua mabomu hewani, akizungumza mara baada ya zoezi hilo mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Simiyu, mratibu wa Polisi Oscar Felisian amesema lengo la zoezi hilo ni kuwaweka tayari wananchi iwapo patatokea majanga mbalimbali likiwemo suala la ugaidi.
 
Kwa upande wao wananchi waliozungumza na ITV kuhusuina na zoezi hilo wamelipongeza jeshi hilo huku wakiliomba liwe linafanya zoezi hilo mara kwa mara ili wananchi waweze kuwa na uelewa.
 
Hilo ni zoezi la kwanza kutekelezwa na jeshi la polisi tangia kuanzishwa kwa mkoa huu.
 

No comments:

Post a Comment

PESA YAIMBA WIMBO