Friday, November 20, 2015

Zaidi ya wakazi 3000 kijiji cha Mwasonge hawana mawasiliano na jiji la Mwanza.

Zaidi ya wakazi 3000 wa kijiji cha Mwasonge katika wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, wakiwemo wanafunzi wa shule ya msingi ya kijiji hicho pamoja na akinamama wajawazito wanalazimika kuvuka kwa mtumbwi kwenda katika eneo la Buhongwa jijini Mwanza kupata huduma za kijamii baada ya daraja la mto nyashishi kukatika na kusombwa na maji.
Hii ndiyo hali ya usafiri wa kila siku kwa wakazi wa kijiji hiki kilichopo mpakani mwa wilaya ya Nyamagana na Misungwi.
 
Wakazi wa kijiji hiki wanaizungumziaje hali hii?  
 
Mmiliki wa mtumbwi unaotumika kuwavusha wakazi hawa Aloyce Charles anasema changamoto kubwa anayokumbana nayo ni mtumbwi wake kubeba abiria zaidi ya 15 badala ya abiria sita na tishio la kuliwa na mamba. 
 
ITV imeongea na baadhi ya viongozi wa serikali ya kijiji hicho ambapo wameiomba serikali kuwajengea daraja kubwa litakalohimili uwezo wa magari na waenda kwa miguu, kwani umbali kati ya Mwasonge hadi Buhongwa ni kilometa nne tu, tofauti na kupitia njia ya Usagara hadi Mwasonge ambako ni umbali wa kilometa 20.
 

No comments:

Post a Comment

PESA YAIMBA WIMBO