Friday, November 20, 2015

Bodi ya mikopo ya elimu ya juu yakamilisha utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza.



Licha ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu imesema imekamilisha zoezi la utoaji mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza, ITV imeshuhudia wanafunzi wengi nje ya bodi hiyo wanaodai kukosa mikopo huku wakiwa na sifa za kupata mikopo.
Ni wiki kadhaa tu baada ya vyuo vya elimu ya juu kufunguliwa nchini, hapa ni nje ya jengo la bodi ya mikopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
 
Wakati serikali ikijiandaa kuanza kutekeleza sera ya elimu bure, nini neno lao kwa rais Dkt John Pombe Magufuli?
 
Maafisa wa bodi ya mikopo wanasema hadi kufikia jana Nove 19 zaidi ya sh bilioni 196 zimepangwa kuwanufaisha wanafunzi 52746 wenye vigezo kwa mwaka wa masomo 2015/16.
 

No comments:

Post a Comment

PESA YAIMBA WIMBO