Friday, November 20, 2015

Afya za wahanga wa ajali ya mgodi wa Nyangarata zinazidi kuimarika.

Siku tano baada ya wahanga wa ajali ya mgodi wa Nyangalata kufikishwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama afya zao zinaendelea vizuri huku wakianza kufanya mazoezi ya kutembea na kula vyakula vya kawaida kwa maelekezo ya daktari anayewahudumia.
ITV imetembelea katika hospitali ya wilaya ya Kahama na kuzungumza kwa nyakati tofauti na wahanga hao huku wakionyesha nyuso za furaha na wakimshukuru mwenyezi mungu kwa miujiza aliyowatendea kwa siku 41 na hatua waliyofikia sasa.
 
Aidha mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Kahama Dr.Joseph Ngowi amesema afya za wagonjwa wote watano zinaendelea vizuri ila kwa mujibu wa vipimo imebainika baadhi yao wamepata nimonia kutokana na baridi kali chini ya mgodi pamoja na kukosa hewa safi kwa muda mrefu lakini baada ya siku 21 huenda wakaanza kuruhusiwa kwenda makwao.
 
Kwa upande wao baadhi ya ndugu wa wahanga hao wameeleza jinsi wanavyojisikia furaha ndugu zao kupatikana wakiwa hai huku wengine wakieleza hali ilivyokuwa baada ya tukio la ajali na sasa baada ya ndugu zao kupatikana hai.
 

No comments:

Post a Comment

PESA YAIMBA WIMBO