Friday, November 20, 2015

Rais Dk Magufuli alizindua bunge la 11 na kuainisha vipaumbele vya serikali yake.

Rais Dk Magufuli alizindua bunge la 11 na kuainisha vipaumbele vya serikali yake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Magufuli amelizindua bunge la kumi na moja na kuainisha vipaumbele vya Serikali ya awamu ya tano huku wapinzani wakitoka nje kususia hotuba hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bunge hilo,Mhe.Dr.Magufuli amesema vipaumbele vikuu vya Serikali yake ni kupunguza urasimu katika nyanja zote,kubana matumizi,nidhamu ya mali za Serikali pamoja  na uwajibikaji kwa watumishi wa umma.
 
Aidh Dr.Magufuli amesema azma yake ya elimu bure hadi kidato cha nne ipo pale pale na kuanzia mwakani amepiga marufuku mchango wa aina yoyote kwa shule za umma ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa hilo.
 
Pia amezungumzia mikakati yake ya kutekeleza kivitendo azma ya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati.
 
Naye waziri mkuu Khasim Majaliwa amesema watumishi wa Serikali ambao wataonekana kuwa kikwazo kwa Serikali hiyo ya awamu ya tano wataoona cha moto.
Awali bungeni hapo ilijitokeza hali ya sintofahamu iliyomlazimu Spika wa Bunge Job Ndugai kuamuru wabunge waliohusika na sintofahamu hiyo watoke nje ya eneo la bunge.
 

No comments:

Post a Comment

PESA YAIMBA WIMBO