Friday, November 20, 2015

Mganga mkuu wa Kagera Dkt.Rutachunzibwa athibitisha kuzuka kwa ugonjwa wa kipindupindu.

Mganga mkuu wa mkoa wa Kagera Dkt. Thomas Rutachunzibwa leo amethibitisha kuzuka kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika mkoa huo na hivyo ametoa tahadhali kwa wananchi na kuwataka wazingatia suala la usafi ili wajiepushe na ugonjwa huo unaoenea kwa kasi.
Akizumngumza na waandishi wa habari mganga huyo mkuu amesema ugonjwa huo umethibika kufuatia matokea ya vipimo vya maabara vya wagonjwa watano waliokuwa miongoni mwa wagonjwa waliolazwa katika zahanati ya nshambya iliyoko katika manispa ya Bukoba kwa ugonjwa ambao ulikuwa haujajulikana wa kutapika na kuharisha. 
 
ITV haikuishia hapo ilifika katika kambi ya zahanati ya Nshambya ambayo ni maalumu kwa kuwapokea, kuwalaza na kuwapa matibabu wanaokubwa na mlipuko wa ugonjwa kipindupindu, katika kambi hiyo baadhi ya wagonjwa walizungumza wanaeleza walikumbana na ugonjwa huo.
 
Naye Felista Rweyemamu mganga wa zahanati ya Nshamba ambaye ni mkuu wa kambi hiyo anaelezea hali ya wagonjwa wanaoletwa katika kambi hiyo kwa ajili ya kupata matibabu, huku, Valentine Rujwahuka afisa muuguzi wa zahanati akieleza changamoto wanazokumbana nazo katika kutoa huduma kwa wagonjwa wa kipindipindu.
 

No comments:

Post a Comment

PESA YAIMBA WIMBO