#Habari Rais wa awamu ya tano Dk.Magufuli amesema kwamba utoaji wa elimu bure kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari kwa serikali yake ni wenye dhamira ya kweli kwa wanafunzi kutolipa michango ya aina yeyote ile tofauti nailivyokuwa ikisemwa kwani hiyo ni azma wakati wa kampeni kwa watanzania na kuahidi kuwa wanafunzi wa elimu ya juu chini ya serikali yake watapewa mikopo kwa wakati unaostahili.

#Habari:Rais Dk.Magufuli amesema kuwa kiu yake nikuhakikisha kwamba uchumi wa kipato chakati unafanana na maisha halisi ya wananchi wa Tanzania ili nchi na watanzania wafurahie matunda ya taifa lake,huku akisema kuwa waliobinafsisha viwanda kuhakikisha kuwa wanawajibishwe kwani serikali yake toka mwanzo alisema ni ya viwanda ili kila kitu kizalishwe hapa nawatu wafurahie soko la ndani na kuzalisha ajira nyingi ifikapo 2020.

Licha ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu imesema imekamilisha zoezi la utoaji mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza, ITV imeshuhudia wanafunzi wengi nje ya bodi hiyo wanaodai kukosa mikopo huku wakiwa na sifa za kupata mikopo.
Ni wiki kadhaa tu baada ya vyuo vya elimu ya juu kufunguliwa nchini, hapa ni nje ya jengo la bodi ya mikopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Wakati serikali ikijiandaa kuanza kutekeleza sera ya elimu bure, nini neno lao kwa rais Dkt John Pombe Magufuli?
Maafisa wa bodi ya mikopo wanasema hadi kufikia jana Nove 19 zaidi ya sh bilioni 196 zimepangwa kuwanufaisha wanafunzi 52746 wenye vigezo kwa mwaka wa masomo 2015/16.

No comments:
Post a Comment