Watu watano wamepoteza maisha katika ajali iliyotokea leo March 29, 2018
jioni katika maeneo ya Kasharazi ulipo Mlima wa K9 {K’nine} mkoani
Kagera baada ya gari lililokuwa likisafirisha wakimbizi kutoka Kigoma
kuelekea Burundi kugongana na gari lingine na kusababisha vifo vya watu
hao.
Kamanda wa Polisi Kagera Augustine Ollom
amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na amesema yapo magari mawili
yaliyokuwa yakiwasafirisha wakimbizi kurudi nchini kwao, yalipata ajali
baada ya Bus moja kugonga lingine na kusababisha vifo vya watu watano na
majeruhi.
Ameyataja magari hayo kuwa lipo gari lenye namba za usajili T331 DFV aina ya YUTONG liligonga Bus T765 DLD
aina ya TATA ambapo lilipoteza uelekeo na kumgonga mwendesha Baiskeli
na akafariki palepale, kati ya hao wengine waliopoteza maisha ambao
majina yao bado hayajatambulika wapo wakiume wawili na wa kike wawili.
No comments:
Post a Comment