Wednesday, December 2, 2015

Natumai Hujambo,

Natumai Hujambo,
Katika Dira ya dunia Jioni hii nakualika kuungana nasi kwenye mjadala wa wiki tukiangazia suala la Ufisadi barani Afrika. Kulingana na utafiti uliofanyika hivi karibuni na shirika la kuchunguza ufisadi duniani -Transparency International raia mmoja kati ya watano barani Afrika hutoa hongo. Ufisadi umekuwa ni jambo linalowakera wengi, lakini umeendelea kuwepo, licha ya kwamba mikakati mbali mbali imekua ikiwekwa kuukabili. Hii leo tunauliza je Juhudi zilizopo za kupambana na ufisadi barani Afrika zinatosha? Tupe maoni yako, je unadhani wewe binafsi pia unamchango gani katika kupambana na ufisadi?. Pamoja!

No comments:

Post a Comment

PESA YAIMBA WIMBO