
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Faraji Said Champunga (45), mkazi wa kijiji cha Kasisi B, amefariki duni kwa kupigwa na radi huku wawili wakijeruhiwa, katika mazingira ya kutatanisha kutokana na kutokuwepo na mvua, huku katika mazingira hayo hayo, katika kijiji cha Ilolangulu kusini kondoo wawili wakipoteza maisha kwa kupigwa na radi hiyohiyo, tukio lililotokea katika wilaya ya Uyui mkoani Tabora.
Wakiongea kwa masikitiko katika eneo la tukio hilo lililopoteza maisha ya kijana aliyekuwa akitegemewa kama fundi wa pikipiki za boda boda, mashuhuda wa tukio hilo katika kijiji hicho, huku wakimwachia mungu tukio hilo wamesema kuwa, haijawahi kutokea hali kama hiyo radi kupiga mtu wakati mvua ikiwa hainyeshi.
Akizungumzia kupigwa radi kondoo wawili na kufa papo hapo, mwenyekiti wa kijiji cha Ilolangulu kusini Bw. Nasiro Wira amesema kuwa, taarifa za kupigwa radi kondoo hao zimewaacha katika kitendawili kutokana na mvua kunyesha kijiji cha pili.
Akizungumza na wananchi hao katika matayarisho ya mazishi ya marehemu Faraji Said mwennyekiti mteule wa halmashauri ya wilaya ya Uyui Bw, Saidi Ntahondi amewataka wananchi, katika matukio kama hayo wawe watulivu na wasiyahusishe na imani potofu, kwani inaweza kuondoa amani na utulivu, katika jamii.
No comments:
Post a Comment