Sunday, December 6, 2015

Mbogo wanane wamegongwa hadi kufa na wangine kujeruhiwa vibaya katika ajali ya gari iliyotokea katikati ya hifadhi ya taifa ya mikumi barabara ya morogoro iringa baada ya dereva wa lori aina ya fuso kushindwa kulimudu gari hilo wakati kundi la mbogo hao wakivuka barabara. ITV imeshuhudia mbogo hao wakiwa wamegongwa katika hifadhi ya Mikumi ambapo mashuhuda wa tukio hilo wamesema ajali hiyo imetokea majira ya saa tatu usiku wakati gari hilo likitokea Mang`ula wilayani kilombero kuelekea jijini Dar es Salaam ambapo wameliomba jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kuimarisha doria hasa wakati wa usiku katika hifadhi hiyo.

No comments:

Post a Comment

PESA YAIMBA WIMBO