Sehemu ya 11
RIWAYA: ROMEO & JULIETH
MTUNZI: richard R. MWAMBE
MAHALI: LINDI - NANGUMBU
Simu: (whatsapp) +255 767 152125
email: amatagaimba@gmail.com
twitter: Richard Ric Mwambe
SKYPE: Richard Mwambe
MTUNZI: richard R. MWAMBE
MAHALI: LINDI - NANGUMBU
Simu: (whatsapp) +255 767 152125
email: amatagaimba@gmail.com
twitter: Richard Ric Mwambe
SKYPE: Richard Mwambe
CHAPISHO LA 11
NYAKATI ZA PENZI LA MAIKO NA AMANDA.... endelea
11
Maiko alikuwa akimwangalia sana Amanda, mpaka Amanda alihisi aibu kiasi Fulani.
“Mbona waniangalia hivyo?” Amanda aliuliza
“Aaa naustaajabu uzuri wako, nahisi kama ulipendelewa kuumbwa” Maiko alijibu kwa maneno ya utani.
“Mh! Mzuri ntakuwa mimi?” Amanda aliongeza.
“Ee, mwanaume akikusifu kuwa wewe ni mzuri basi ujue ni mzuri kwelikweli,” akainua kinywaji chake na kupiga funda moja kisha akaitua mezani na kuendelea, “Amanda una mpenzi au mchumba?”
Amanda alionekana kushtushwa kidogo na swali lile, akatabasamu na kuruhusu tena vile vishimo mashavuni mwake, hakujua kama kwa kitendo hicho anamuumiza sana Maiko kwani huo ni ugonjwa wake mkubwa.
“Sina Maiko, vipi kwani?” Amanda alihoji
“Ah, hata kama nilitaka kuwa padri lakini nahisi mabadiliko, sasa nahitaji kuwa na wewe mrembo kama hutojali” Maiko alitupa karata yake kwa mtindo huo. Amanda alitulia kimya akiangalia chini huku akichezesha mguu wake wa kushoto ka kuutembezambeza sakafuni, Maiko alikuwa bado ametulia akisubiri nini kitatoka kinywani mwa Amanda. Amanda alinyanyua uso wake na kumtazama Maiko.
“Ninyi wanaume ni waongo sana” Amanda alianza kwa lawama
“Hapana, si wote, ni wachache sana waongo, lakini hii inapelekea kuwa hivi kutokana na ninui wenyewe kuukubali uongo kuliko ukweli” baada ya Maiko kusema hivo wote waliangua kicheko na kugonga viganja vya mikono yao.
“Sina mpenzi wala mchumba, unasemaje?” Amanda aliuliza.
Amanda alimtazama Maiko kwa jicho tata lililomfanya Maiko ajikute anashindwa kumtazama Amanda na kupeleka macho yake pembeni kabisa.
* * *
Penzi changa liliamka kwa Maiko na Amanda, Maiko alimpenda sana Amanda na Amanda vivyo hivyo. Zawadi za hapa na pale zilikuwa si haba kwa wawili hao. Wapo waliomsifu Maiko kwa kupata msichana mrembo kama huyo, na wapo waliomuonea wivu.
Maiko alimtambulisha Amanda nyumbani kwao, wazazi wa Maiko na ndugu zake walimpenda Amanda na kumsifia kwa mengi, daima Amanda alikuwa huru kwenda kwa kina Maiko muda wowote na alipokelewa kwa mikono miwili na familia ya Maiko, naye alijisikia furaha sana kwa hilo, alijisikia nyumbani, mara nyingi alipokwenda alibeba japo zawadi kidogo kwa ajili ya wazazi wa Maiko, wazaa chema.
Ilikuwa ni mazoea yaliyojengeka hata wazazi wa maiko waliweka tick kwenye uhusiano huo na kumsifu kijana wao kuwa anajua kuchagua.
Upande wa pili wa shilingi…
Amanda aliwashirikisha wazazi wake juu ya uhusiano wake na Maiko, haikuingia kichwani kwa baba wa Amanda kwani alionekana wazi kuwa ni jinsi gain alikuwa amechukia kupokea habari hiyo ambayo kwake tuingeiita mbaya, alimtazama binti yake kwa jicho kali sana,
“Nahisi umeanza kurukwa na akili eti?” baba wa Amanda aliuliza, “Sisi wazazi wako ndiyo tunaojua mchumba mzuri anaekufaa wewe, sio we kujichagulia tu huko na huko halafu utuletee mabalaa,”
Amanda alibaki kimya hakujibu neno.
“Lakini baba, mi ndiye nimempenda,” Amanda alisisitiza, kitendo kilichozidi kumchefua baba yake.
“Narudia tena, sisi wazazi wako ndiyo tunaojua mchumba wako ni nani!, usitupangie wewe,” baada ya kusema hayo baba wa Amanda alinyanyuka na kumuwacha Amanda akilia huku mama yake akijaribu kumbembeleza.
Amanda aliumia sana kwa kitendo cha baba yake kumkatalia katakata swala la yeye kuwa na mahusiano na Maiko kwa kigezo kuwa wao kama wazazi wanajua nani wa kuwa mchumba wake, baba wa Amanda bado alikuwa kashika mila za kumchagulia binti mchumba, mila za kizamani, mila zilizosababisha wasichana wengi kuishi kwa taabu katika ndoa zao, kuolewa na watu wasio mioyoni mwao. Mama wa Amanda alimbembeleza sana Amanda na kumuahidi kuwa ataliongea hilo swala na baba yake ili walimalize, hapo Amanda aliona ahuweni kidogo.
Amanda alimpenda sana Maiko, Maiko alikuwa kila kitu kwake, mapenzi motomoto yalikuwa kati wawili hao, ilikuwa ngumu sana kukaa siku mbili bila kuonana, kitendo cha baba wa Amanda kilianza kumpa wakati mgumu Amanda, kilimharibia kesho yake.
* * *
Amanda na Maiko walikuwa wameketi katika moja ya grosari zilizopo katika barabara ya Shauri moyo pembezoni kabisa mwa ukuta wa shule ya Al-Haramain wakiwa na kinywaji baridi katikati yao. Maiko alionekana kuwa mtu mwenye mawazo mengi sana wakati Amanda yeye alionekana katika hali ya kutojielewa. Maiko akamwangalia Amanda, kwa upole akamuuliza
“Kwa hiyo, mipango yetu yote inakufa?”
“Mimi sijui nifanyeje my love, nakupenda Maiko nakupenda sana lakini baba hataki kabisa” Amanda alijibu huku chozi likimdondoka.
Maiko alimshika Amanda mikono yake na viganja vyao vikawa pamoja,
“Amanda, unanipenda kweli?” akamuuliza
“Nakupenda Maiko, sijawahi kupenda namna hii” Amanda alijibu
“Nami nakupenda pia, na sipendi kukupoteza maishani, wewe ni msichana wa maisha yangu, hakuna atakayetutenganisha, au we unasemaje?” maiko aliuliza
“Napenda iwe hivyo, lakini je itawezekana?” Amanda aliuliza.
“Kwa nini isiwezekane? Kama mimi na wewe tumeamua hakika itawezekana”
Baada ya kuzungumza machache wawili hao waliondoka eneo hilo, ilikuwa tayari imetimu saa moja ya usiku, Maiko alimshawishi Amanda waende hadi anakoishi japo akapaone tu maana tangu waanze uhusiano wao miezi kadhaa nyuma Amanda hakuwahi kufika anapoishi Maiko isipokuwa mara nyingi alifika kwa wazazi wa Maiko. Baada ya mvutano kidogo kwa kuwa Amanda alikuwa akikataa kwenda kwa madai kuwa ni usiku sana, alikubali ila akaomba kukaa nusu saa tu. Haikuwachukua muda mrefu walikuwa tayari wamefika, chumba kimoja kidogo cha Maiko chenye kitanda tu ndani yake,
“Vipi, mbona unaonekana kama waogopa?” Maiko alimuuliza
“Lazima niogope, kuingia kwa chumbani kwa mwanaume hujui hatari yake?” alijibu kwa kuuliza
“Ah, hakuna hatari yoyote wasiwasi wako tu, njoo uketi japo ni kitandani,” Maiko alimkaribisha Amanda kuketi huku akimvuta mkono wake kwa mahaba, Amanda kwa hatua za kivivu alikisogelea kile kitanda na kuketi juu yake.
“Ewaaaaa mke wangu mtarajiwa sasa ameketi kitandani mwangu!” maiko alizungumza kwa utaratibu sana sentensi hiyo iliyomfanya Amanda kucheka.
Jioni hiyo manyunyu ya mvua yalianza kuligonga bati la nyumba aliyopanga Maiko, Amanda alianza kuingiwa na hofu juu ya hali hiyo, alimtyazama maiko na kumwambia
“Maiko, mvua, mi naogopa kuchelewa nyumbani nipeleke tafadhali,”
Maiko alimtazama Amanda na kumuuliza
“Sasa unataka kuniacha peke yangu na hali hii mpenzi?”
Amanda alitulia tuli, baada ya sekunde kadhaa alinyayuka na kuuendea mlango, radi kali iliyotengeneza mwanga mkali angani ilimfanya Amanda kurudi ndani na kujitupa kitandani kwa Maiko huku akipiga kelele, mvua ikaanza kunyesha na upepo mkali kuifuatia. Maiko alimuendea Amanda pale kitandani na kumtazama usoni,
“We vipi?” alimuuliza
“Naogopa radi mimi” alijibu Amanda. Mara umeme ukakatika giza likatawala nchi, Maiko hakuwa na mshumaa, aliichukua taa ya ke ya kichina ya kuchaji na kuiwasha lakini ilitoa mwanga hafifu sana ilikuwa haijachajiwa muda mrefu, sekunde chache ikazimika, giza likakijaza chumba kile, Maiko alihisi Amanda akitetemeka sana, akajilaza kitandani na kumkumbatia, mkono wake wa kushoto ukipita juu ya kiuno cha binti huyo, msisimko mkali ukamuingia Amanda ukizingatia maeneo hayo ndiyo yale yenye mtekenyo mkali mwilini mwake.
Amanda alitulia pale kitandani huku kalala kifudifudi, kimya, mkono wa Maiko ulikuwa ukiendelea kutalii kiuno cha binti huyo, shanga zilizokizunguka zilimpa wakati mgumu Maiko.
Kutoka kiunoni mkono ule ulitambaa kuelekea mgongoni, Amanda alitoa miguno hafifu wakati akiufanyia ukarimu wa utulivu mkono wa Maiko ambao ulikuwa ndani ya blauzi yake. Maiko alshusha pumzi ndefu na kumtekenya Amanda, kitendo kilichomfanya Amanda ashtuke na kujigeuza kuangalia, sasa akawa amelala chali. Giza liliwafanya kutokuonana sawasawa, Amanda aliuchukua mkono wa Maiko na kuuweka kitovuni kwake huku asikika kutoa mihemo ya haraka haraka, Maiko aliendelea na shughuli hiyo huku mvua ikiendelea kunyesha, sasa ilikuwa ni kubwa mno, radi kali ilipiga na kumfanya Amanda amvutia Maiko kitandani kwa woga na wote wakajikuta wamekumbatiana kwa nguvu, huku nyuso zao zikielekeana,
“Nakupenda Amanda,” maiko alitamka
“Nakupenda Maiko,” naye alijibu, kisha midomo yao ikakutana mchezo wa kunyonyana ndimi ukachukua nafasi huku kila mmoja akishika sehemu za mwenza kiufundi na mahaba makubwa.
* * *
Amanda alikurupuka kitandani na kumsukumia maiko upande wa pili, akaanza kuhema kwa nguvu kama mtu aliyekuwa akikimbizwa. Alinyanyuka pale kitandani akiwa kama alivyozaliwa baada ya ule mchezo mtamu aliokuwa akiufanya na Maiko, akaiendea stuli ndogo na kuchukua simu ya Maiko kutazama muda, lo, ilikuwa saa sita kasoro robo usiku, Amanda akajawa na hofu, atamueleza nini baba yake, alikuwa wapi, na nani.
“Maiko, nimekwisha!” alilalama
“Nini Amanda?” maiko aliuliza huku akinyanyuka kitandani naye akiwa katika hali ileile.
“Ni saa sita kasoro usiku sasa Maiko nitarudije nyumbani?” Amanda alieleza.
“Amanda,” Maiko aliita huku akisimama na kumuendea Amanda pale alipokuwa amesimama, “Nini shida beibi?” akamuuliza.
“Saa sita kasoro sasa Maiko,” Amanda alijibu huku akilia.
“Basi nyamaza mpenzi” Maiko alimfuta machozi kwa kiganja chake, “Tazama mvua isiyotaka kukatika, unafikiri utaendaje nyumbani? Hata wazazi wako hawatalaumu kukuona sasa kwa maana wanaona hali halisi ya huko nje” maiko alimfariji Amanda.
“Nikodie Tax baba yangu atalipa,” alimwambia Maiko.
Mapigo ya moyo ya Amanda yalikwenda mbio kwa hofu ya kuchelewa nyumbani. Tax ilifika, Maiko na Amanda waliingia na kuondoka, bado mvua ilikuwa ikiendelea kunyesha.
“Vipi mbona huongei?” Maiko alianzisha mazungumzo
“Ah! Nawaza hapa huko home itakuwaje leo” Amanda alijibu.
Kutokana na mvua iliwachukua kama lisaa limoja kufika kwa kina Amanda, Amanda alishuka na kuuendea mlango wa mbele wa nyumba yao na kugonga kwa fujo. Mara mlango ulifunguliwa na Amanda alikutana uso kwa uso na baba yake, wakabaki wakitazamana.
Amanda aliingia ndani na baba yake akampisha kisha akaufunga mlango nyuma yake.
“Amanda!” baba aliita, Amanda kwa kusikia sauti hiyo alitamani hata kuanguka maana alikuwa akitetemeka kwa woga, akageuka kumtazama baba yake.
“Pole kwa mvua, nenda kapumzike” alimweleza binti yake. Amanda hakuamini, alijua kuwa sasa ndio kunakucha, aliingia chumbani na kujifungia, jambo la kwanza aliishusha kalenda yake ukutani na kuanza kuhesabu tarehe….
::::BABA WA AMANDA ATAFANYA NINI KWA BINTI YAKE?
:::::KWA NINI AMANDA ANAHESABU TAREHE?
:::::NINI KILIWATENGANISHA MAIKO NA AMANDA KATIKA MAPENZI YAO?

No comments:
Post a Comment