ALICE THE SUPER STAR 23
NA HUSSEIN O. MOLITO
0718 97 56 59
0765 68 48 70
NA HUSSEIN O. MOLITO
0718 97 56 59
0765 68 48 70
“vipi kuhusu filamu yetu?” aliuliza Alice huku akimuangalia mpenzi wake ambae alikua anatabasamu wakati huo.
“nimekuruhusu pia iingie sokoni… nahitaji kukutengenezea furaha na kupandisha kiwango cha mapenzi yakiyopungua kwa ujinga wangu.” Aliongea Brayton na kumfanya Alice amkumbatie na kumbusu busu kwa furaha.
“ok.. Fanya mawasiliano nae basi...ili asikose.” aliongea Brayton na kuingia chumbani.
“ok my husband to be.” aliongea Alice kwa sauti ya kudeka.
*************************
Mualiko wa Alice na mpenzi wake ulipokelewa vizuri na Larry. Hakusita kufika nyumbani kwa kina Alice na kuingia ndani. Alikuta kumepambwa vizuri kamavile kulikua na ujio wa mgeni kutokea nje ya nchi au kiongozi fulani wa serekalini.
Walikaa meza moja na kupata chakula hicho cha mchana kilichochafua meza.
“karibu sana Larry. Jisikie upo nyumbani.” aliongea Brayton baada ya kuona kimya kimetawala.
“nimeshakaribia.” alijibu Larry na kuendelea kula huku macho yake yakiwa chini bila kumtazama yeyote.
Baada ya kumaliza kula, Walikaa kwenye sofa na kubadilishana mawazo.
“niseme tu ukweli Larry... Kwenye movie yenu umecheza kwa kiwango kikubwa sana. Yaani sikuamini nilipoambiwa kua ndio movie yako ya kwanza kucheza...hongera sana.” aliongea Brayton na kumshika shika Alice ambaye alikua amekaa karibu naye.
Larry alijifanya haoni kitendo hicho na badala yake alikua bize na tv ili kukwepesha macho yake kuona yaliyokua yakiendelea kwa wawili hao.
“nashukuru... Mimi mwenyewe bado naona nimecheza chini ya kiwango... Nataka movie nyingine nikamue zaidi ya pale.” aliongea Larry huku akiwapa masikio pekee lakini macho yote yalikua kwenye Tv.
“nini malengo yako kwa sasa... Maana unakaribia kuwa star?” aliongea Brayton.
“kwa sasa najiangalia tu ili kujua ni kitu gani kingine ninachoweza kufanya ili nisiporomoke hapa nilipo. Napenda sana jina langu likue pamoja na mafanikio yangu. Kwani jina likitangulia bila fedha,...nitaishi kwa shida. Maana nitakua naigiza maisha wakati kuikwelli sijafikia level hizo.” aliongea Larry na kuwaibia kidogo kuangalia ili wasije wakafikiri kua anawaonea wivu.
Safari hii alimuona Alice amelala kabisa kwenye kifua cha mpenzi wake huku Brayton akizichezea nywele za Alice. Ghafla wivu wa mapenzi kwa Alice ukaja tena na kumfanya atamani kuaga. Ila alipiga moyo konde na kufikiria kua atakua ameonyesha udhaifu.
Alitulia kimya na kuanza luwaangalia bila kuangalia pembeni mpaka Alice alipokutanisha macho yake na Larry, aligundua kua alikua anamuumiza Larry na kuamua kunyayuka.
Baada ya maongezi machache, Larry aliaga na kuondoka zake.
Hakujua kua dhamira ya Alice na mpenzi wake ilikua ni nini katika mualiko wao. Kwani haukuishia kwa furaha upande wake. Badala yake ulimfanya ajisikie ameonewa kwa kulingishiwa mtu anayempenda na kumuona akipetiwa na mtu mwengine.
Wakati anawaza, simu yake iiita na jina la Alice likajitokeza kwenye kioo cha simu yake.
Hakuipokea kwa mara kadhaa, baada ya kona Alice anazidi kupiga simu, ndipo alioamua kuipokea.
“sorry Larry... Najua kwanini hupokei simu yangu kwa yale yote uliyoyashuhudia... Halikua kusudio langu wewe uumie. Ila hata mimi nimekwazika kwa jinsi alivyokua akifanya mpenzi wangu. Ili kulinda tu ukaribu wetu na kumuhakikishia kua hisia zake juu ya mimi na wewe kuwa wapenzi zimuondoke na asifikirie tena hilo swala, ndio maana ukaona kama vile nilikua pamoja nae. Ila kusema ukweli hata mimi nimejisikia vibaya sana ...amini hivyo Larry.” aliongea Alice na kumfanya Larry kuwa msikilizaji tu. Larry alivuta pumzi ndefu na kumjibu.
“sawa... Ila tambua kua mimi sitaweza kuja tena nyumbani kwako kwa mualiko wowote ule. Hivyo mtakapofikiria kunialika tena, sitakuja.” aliongea Larry na kukata simu.
Alice alijua kabisa ni jinsi gani Larry alivyoumia kwa tukio lile. Hakujua dhamira ya Brayton kama kumualika Larry ilikua kwa ajili ya kumuumiza tu.
Zilipita wiki tatu baada ya kubandikwa posters za filamu ya The Memory na tarehe ya uzinduz ilifika. Watu wengi waliokua na kiu na filamu hiyo walihdhuria na wengine wakasubiri DVD zilizoanza kuuzwa kama njugu baada tu ya uzinduzi.
Kila aliyebahatika kuiona filamu hiyo, alikiri uwezo wa Larry japo kua ilikua ndio movie yake ya kwanza.
Kutokana na kampuni ya Alice the super star kujulikana Afrika nzima, movie hiyo haikuishia Tanzania peke yake, ilisambaa afrika nzima na baadhi ya nchi za ng`ambo ambaqzo zilikua zinapenda pia kuangalia filamu za kiswahili.
Jina La Larry lilianza kuwa gumzo midomoni mwa watu. Wengi waliokua wakiijua historia yake ya maisha walibaki wameachama midomo na hawakuamini kua ipo siku Larry angefikia kiwango alichofikia hivi sasa.
Zuwena ambaye kwa sasa ameshaolewa na ana mtoto mmoja, aliiangalia hiyo movie na kuujikuta akicheka chini chini. Kwani alifahamu kabisa kua hiyo story ilikua inalenga kabisa maisha yake na Larry walipokua wakiishi pamoja miaka mitano iliyopita.
“mungu amsaidie atimize malengo yake.”
Aliongea kimoyo moyo Zuwena ili mume wake asije kusikia. Maana walikua wanatazama wote hiyo movie.
Rafiki yake wa gereji alifurahi sana baada ya kuona kazi ya rafiki yake aliyempokea na kuanza kubangaiza wote kwenye ofisi yake ndogo ya spare za magari na baadae kukua na kuwa gereji ndogo iliyokua ikiaminika na wamiliki wengi wa magari.
“dua zangu zinafanya kazi mdogo wangu...sema ukibadilisha namba usinikose kwenye namba yako mpya.” aliongea rafiki yake Larry.
“kwanini nibadiliishe namba rafiki yangu?” Aliuliza Larry huku akicheka.
“wewe hujijui kua umeshakua star. Tena zile ndoto zako za kuwa karibu na Alice zimetimia... Sema lile denda mwishoni mzee umelikamua.” aliongea Rafiki yake kiutani.
“haya bwana... Nikipata muda nitakuja hapo tupige story.” aliongea Larry na kukaa simu baada ya rafiki yake kuitikia.
Waandishi wa habari walimtembelea Larry nyumbani kwake na kumuhoji baada ya kumhoji Alice.
“nimejisikia furaha sana kucheza na star mkubwa kama Alice. Nadhani ndio naweza sema kuwa ndio siri ya mafanikio yangu. Pia ile hadithi ya filamu nzima ni ni based on true story. Ndio maana nilikua kama narudia kuigiza maisha yangu ya nyuma. Ndio maana ikawa rahisi kwangu au kufanya kwa hisia kali kwa sababu maumivu yake bado hayajapoa mpaka sasa.”
Aliongea Larry alipokua akijibu swali la mmoja wa waandishi wa habari baada ya kuulizwa siri ya mafanikio yake ya kufanya vizuri kwenye mvie yake ya kwanza.
“tunakutakia mafanikio mema katika tasnia hii ya filamu na ahsante kwa ushirikiano wako kwetu sisi waandishi wa habari.”
Waliongea waandishi wa habari baada ya kuridhika na mahojiano waliyofanya na Larry.
Baada ya waandishi wa habari kuondoka, simu yake iliingia sms ya Alice.
“mgao umeshatoka... Fedha zako zipo kwenye account yako nimeshakuingizia.”
Sms hiyo ndio iliyomfana ampigie simu.
“kwa hiyo unataka kuniambia kua now naweza kwenda kuangalia kiasi cha fedha kilichoingia?... Au kama vipi si unitajie tu.” aliongea Larry huku akionekana kua mwenye furaha sana.
“nina imani kua utashangaa...ila nimeamua tu kutimiza ahadi. Amini kuwa fedha utakayo iona ni asilimia 40 ya mauzo yote ya movie.” aliongea Alice na kuzidi kumtia hamu Larry ya kwe nda kwenye ATM ili aangalie kiasi cha fedha alichoingiziwa.
“naona nachelewa wangu.. Acha niende.” aliongea Larry.
“ok”
Alijibu Alice na Larry alikata simu. Hakuchelewa,aliwasha gari yake na kwenda kwenye Atm iliyokua karibu na maeneo aliyopo na kingiza kadi yake na kuangalia salio.
“OH MY GOD......MILIONI MIA MOJA HAMSINI...ZOTE ZANGU?”
Alishangaa sana Larry baada ya kuona salio limemsomea milioni 151 kutokana na salio lake alilokua amelihifadhi benk liolikua milioni mmoja hapo awali.
ITAENDELEA

No comments:
Post a Comment