Friday, December 16, 2016

SIMULIZI: MY DIARY
SEHEMU YA 2
Nilikuwa hata sijajitambulisha kwani nilitaka mjue asili ya majina yangu maana kiukweli nilikuwa na majina mengi kabla na baada ya kuwa superstar. Ila nitatumia jina langu la asili nililopewa na wazazi wangu. Nilipozaliwa tu wazazi wangu waliniita Leah. Ni mtoto wa kimbulu niliyechanganya damu na mama wa kiharabu.Nina historia ndefu sana ambayo kiukweli inahuzunisha sana. Lakini kwa kuwa dunia mapito nitaeleza kwa kifupi hasa upande wa mahusianao na mapenzi. Mimi ni mtoto wa pekee wa kike katika familia ya mzee Bura mzee ambaye alikuwa ni maarufu na tajiri mkubwa pale jijini Arusha.
Ingawa nina mapungufu yangu ya kimaisha lakini kiukweli nimejaliwa uzuri ambao kwa namna moja au nyingine ndo chanzo cha kuharibikiwa na kisha kufanikiwa katika maisha yangu.Ni mweupe kiasi, mwenye umbo la kibantu na nyuma nimefungashia kama mlima kitonga. Nina sura ya mduara kama watoto wa kiharabu ambapo kwa haraka haraka ukikutana na mimi huwezi amini kuwa ni mtanzania tena wa Arusha.
Mungu kanijalia umbo,sura, mwendo, macho na kila kiungo unachojua wewe kinaweza mvutia mwanaume.Ni mnene lakini si ule wa kuboa ni ule wa mpangilio na kwa kweli sina matiti makubwa. Nina macho ya mlegezo ambapo kiukweli nikikuangalia mara mbili ni lazima tu utanitamani. Kasoro yangu kubwa au kilema mungu alichonipa ni kile kilema pendwa yaani kuwa na vijishimo mashavuni mwangu ambapo kila nikicheka vinaonekana.
Leah jina langu la utotoni kwa sasa lishapotea kutokana na matukio yangu. Club za Arusha na sehemu zingine za starehe jijini pale wananijua kama BAMBUCHA. Na jina hili nilipewa siku niliyoshinda taji la miss nyonga. Moshi nilipewa jina la Heinken wowow au Heinken Mutungi baada ya kushinda shindano la bonge kipotabo .Mpaka sasa sijui idadi ya wanaume ambao nishawahi kulala nao ila hawapungui elfu 1. Ndio usishangae kwani kwenye dftari langu la kumbukumbu mwaka jana idadi ya wanaume nilotembea nao walikuwa 892. Sasa ndani ya huu mwaka watakuwa wamezidi elfu lazima. Sipendi na inaniuma sana ila nataka watu wajifunze kutokana na historia hii
Naamini mtanifuatili hadi mwisho ili iwe fundisho kwa wasichana wazuri kama mimi na kwa wanaume wote wanaodanganyika kiurahisi na wasichana warembo. Sitoeleza kila kitu kuhusu maisha yangu lakini nitaeleza vile ninavyovikumbuka na pia ni funzo na fundisho kwa wengine.Nimezaliwa miaka 27 iliyopita huko mkoani Arusha, familia yetu ni moja au miongoni mwa familia tajiri. Kwetu tupo tu wawili mmoja wa kiume na mwingine ndo mimi. Kwa hiyo tupo mimi na kaka yangu tu ambaye na yeye masikini ya mungu maisha yake yaliingia doa hata sijui ni kwa nini familia yetu imekuwa na majanga hivi.
Kwa ufupi japo sitaki kueleza historia yake ila kwa sasa ni shoga na teja. Baba yetu alitupenda sana na alihakikisha tunapata elimu nzuri na bora. Mimi na kaka yangu wote tulisoma International school ya hapo Moshi. Baadaye kaka yangu alianza kuvuta bangi kitu ambacho kilimtia hofu baba yangu na kuamua kumpeleka kusoma nje ya nchi. Alikosea sana kwani alimpeleka south Afrika katika chuo kimoja maarufu cha mambo ya utalii. Huko aliendelaa na tabia yake ya miadarati na mbaya zaidi alianza kuumia madwa ya kulevya hivyo akawa teja kabisa. Akaenda mbali kabisa na kuwa shoga kabisa, sitaki kukueleza zaidi ya hapo kwani lengo la simulizi hii ni kukupa historia ya maisha yangu. Kama nilivyosema mwanzo familia yetu ni tajiri sana kwani baba yangu alikuwa ni mfanyabiashara maarufu wa madini tena yale ya Tanzanite.
Historia ya baba yangu nayo ni ngumu san kwani inasemekana chanzo cha yeye kupata utajiri ni ajali ya wazungu iliyotokea huko Mererani hivyo yeye na wenzake waliiba madini mengi sana. Lakini kabla ya hapo alikuwa ni chokoraa asiye na mbele wala nyuma. Kama nilivyosema sitaki kukupa historia ya watu wengine lakini inanibidi ili uweze kujua aina ya familia ninayotoea. Baba yangu alituambia kuwa yeye alikuwa ni mtoto yatima ambaye baba na mama yake walikufa kwenye ajali mbaya iliyotokea huko Kateshi/mbulu.
Hicho ndicho kikawa chanzo cha yeye kuwa chokoraa. Baadaye alikuja Arusha kutafuta maisha ambapo walipelekwa Mererani kam manyoka. Huko aliteseka sana mpaka alipokuwa kijana anayejitambua. Baadaye ndo akapata bahati ya mtende ya kuiba madini. Tangia hapo akaanza biashara ya kuuza madini na mungu alimjalia sana na baadaye alikuwa anaenda Dubai kuchukua magari.Huko ndipo alipopata bahati ya kukutana na mtoto wa kiharabu ambaye naye alimpata katika hoteli ambayo alikuwa akifikia. Inasemekana msichana huyo alikuwa nimzuri sana kitu ambacho kilimfanya baba yangu atumie gharama kubwa kumpata.
Kwa kuwa binti huyo alikuwa akifanya kazi kwenye hotel hiyo aliyokuwa akifikia hivyo ilikuwa ni rahisi kumwingiza laini. Basi hicho ndo chanzo cha mimi kuzaliwa. Baba yetu alituambia kuwa baada ya mahusiano yao ya mda mrefu na mtoto huyo wa kiarabu huku wakizunguka nchi nyingi na kula raha, baadaye binti huyo aliacha kazi na kuja Tanzania.Baba anasema walipata wakati mgumu sana kwani familia ya binti huyo mrembo alikataa katu katu mwanao kuolewa Afrika na mtu mweusi tena mkristo.
Hivyo basi kutokana na upendo wao wa dhati binti huyo alikubali kutengwa na familia yao na kuja Tanzania na kuja kuishi na baba yangu. Nazani sasa umeanza kupata picha halisi ya uzuri wangu. Huu unene sijui niliupata wapi lakini nahisi ni kwa upande wa baba yangu ambao na wao nasikia walikuwa ni wazuri sana.Hapondipo historia ya maisha yangu inapoanzia.
Nimekulia kwenye familia ya kitajiri hali ambayo ilinifanye nisizijue shida mpaka nilipofkisha umri wa kubalehe. Nakumbuka niliwahi sana kubalehe au kuvunja ungo na kipindi hicho nilikuwa standard six(darasa la sita) huko international school mjini Moshi.Basi waswahili husema hujafa hujaumbika na kaka yangu kama nilivyowaeleza alipelekwa nje ya nchi ambapo baada ya miaka mitatu alirudi nchini akiwa katika hali hiyo ya uteja na ushoga.
Kaka yangu huyu alikuwa ni wa mama mwingine ambaye baba alizaa nae kabla ya kukutana na mama yangu.Najua unasubiri kwa hamau na jamu kujua nini kilitokea katika maisha yangu mpaka mimi kuharibikiwa na kuwa malaya, kahaba maarufu ndani na nje ya nchi.Sio mbaya nikaanzia hapa, ilikuwa ni siku ya jumapili asubuhi mimi mimi nikiwa likizo nimelala kwenye chumba changu, kipindi hicho najielewa kabisa kwani tayari nilikuwa nilikuwa na umri wa miaka 13 na tayari nilishaanza kusoma sekondari.
Siku hiyo ulitokea ugomvi mkubwa sana baina ya mama yangu na baba yangu.Chanzo kikiwa ni mama ambaye alikuwa akimshinikiza baba waame Tanzania na kwenda kuishi Dubai kwenye moja ya jengo lao la kifahari ambalo walikuwa wamelinunua. Baba alikuwa akikataa kwa madai kuwa asingeweza kuhama Arusha kwani biashara zake zingeyumba sana. Ugomvi ulikuwa ni mkubwa sana kitu ambacho kilimpelekea mama yangu kuondoka Tanzania na kurudi kwao Dubai.Kiukweli mpaka leo sina uhakika kuwa hiyo ndo ilikuwa sababu ya msingi ya wao kuachana au kulikuwa na kitu kingine nyuma ya pazia.
Tangia siku hiyo sikuwahi kumwona tena mama yangu mpaka leo hii ninapoamua kusimulia historia ya maisha yangu.Tuliendelea kuishi na baba yetu na cha ajabu baba hakutaka kuoa mwanamke mwingine yeyote.Tuliishi vizuri sana na baba yetu ingawa kaka yangu tayari maisha yake yaliharibika na kuugua ukichaa kabisa.Sikushangaa sana kwani tunajua madhara ya madawa ya kulevya.
Lakini kuna kitu kimoja ambacho huwa nakikumbuka sana. Kitu hicho ni kilichosemwa na daktari mmoja wa KCMC ambaye ni bingwa wa saikolojia na magonjwa ya akili. Alitueleza kuwa kaka yangu alikuwa anaugua ugonjwa wa U-SOCIAL huu ni ugonjwa mbaya sana unaosababishwa na mapenzi.Inasemekana kuwa kaka yangu alipokuwa huko chuoni alitokea kumpenda dada mmoja ambaye ambaye alikuwa amemzidi mwaka mmoja wa masomo.
Inasemekana pia mapenzi yao yalipita kiasi mpaka wakawa kama ni mwili mmoja. Daktari huyo alitueleza kuwa U-SOCIAL ni ugonjwa hatari sana ambao unafanya watu wengi kuchanganyikiwa na kuwa vichaaa kabisa. Dakatri huyo alisema kuwa huo ni upendo mkubwa sana ambao mtu hawezi kuishi bila ya mwenzie na nakumbuka alitutolea mfano wa nyuki ambao wanakuwa tayari kutoa kizazi chao kwa ajili ya nyuki mmoja ambaye ni malikia.
Sijui kama nipo sahihi sana ila mtawauliza wataalam wa ecology. Basi inasemekana kaka yangu na huyo msichana walifikia hatua hiyo kwani kaka yangu alishawahi kumtolea mpaka figo kuokoa masiha yake. Binti huyo alikuwa anatokea Kampala nchini Uganda na kutokana na hali nzuri ya kiuchumi baiana ya familia zote mbili yaani ya kwao na kwetu penzi lao liliweza kushamiri sana.
Kwa kuwa binti huyo alimtangulia kaka yangu mwaka mmoja wa masomo basi alivyomaliza alirudi nchini kwao Uganda. Hapo ndipo kasheshe ilipoanzia kumbe binti yule alikuwa na mpenzi wake wa mda mrefu na ndiye alimpeleka South Afrika kwa ajili ya masomo. Hivo alipomaliza tu masomo aliolewa na kibaya zaidi siku ya harusi yake kaka yangu alipewa taarifa na mmoja wa marafiki wa karibu wa msichana huyo. Kaka yangu akafunga safari mpaka nchini Uganda kwenye mji mkuu wa nchi hiyo na alifikia Severa Hotel sehemu ambayo shughuli za harusi zilikuwa zikiendelea. Hakuamini macho yake lakini ukweli ndo ulibaki huo.
Inasemekana kaka yangu alifanya sana vurugu siku hiyo lakini hazikusaidia kitu kutokana na ulinzi mzuri ulio kuwepo kwenye ofisi hiyo. Basi kwa msaada wa marafiki zake walifanikiwa kumsaidia na kumrudisha nchini south Afrika.Lakini wiki chache baadaye alilazwa kwa kile kilichoitwa jaribio la kutakakujiua. Baadaye aliamua kuiingiza kwenye sakata la kutumia madawa ya kulevya. Kama hiyo haitoshi alianza kupoteza ufahamu wake juu ya maana ya maisha na kila siku ya mungu alikuwa akitafuta faraja yake iliyopotea bila mafanikio. Kwa ufupi hicho ndicho kilichomfanya kaka yangu kuwa shoga , teja na sasa chizi kabisa.
Imenilazimu kuelezea kwa kifupi huu ugonjwa wa U-SOCIAL ili niwape somo ndugu zangu hasa kwa wale wanaopenda kucheza na hisia za wenzao. Ndugu zangu wanaume nawashauri msiwemnapenda kupita kiasi na wasichana jamani tusikubali kuingia kwenye uhusianao na wanaume wengine ili hali wapo ambao tunawapenda kwa dhati. Hayo ni machacahe kwa upande wa kaka yangu sasa turudi upande wangu ambaye ndio tumaini la pekee lililobaki kwa upande wa baba yangu.
Sijisifii lakini kiukweli nilikuwa na uwezo mkubwa darasani kitu ambacho kilimfurahisha sana baba yangu na kuwa tayari kuniudumia kwa gharama yeyote ile. Basi niliendelea kuishi maisha mazuri yale ya kutojua shida, maisha ambayio kila mtu aliyatamani. Nilisoma mpaka nikafika form five hapo ndipo safari yangu ya maisha yalipoanza kuingia doa. Hapa nitasimulia kwa urefu zaidi kwani ndicho chanzo cha mimi kuharibikiwa. Nakumbuka kipindi hicho biashara ya baba zilianza kuyumba, migogoro ya kutokulipa kodi na serikali ilimmaliza.***ITAENDELEA

No comments:

Post a Comment

PESA YAIMBA WIMBO