Nilikuwa nimetoka katika mizunguko yangu jijini, mishe za hapa na pale zinazotuweka hapa mjini Dar es salaam. Nikielekea maskani mji mpya Kigamboni, kufikia mitaa fulani nikamuona akifukua fukua katika jalala, ni kawaida kuwaona watoto wa mitaani wakiwa katika hali kama hiyo na mimi huwa si mtu wa kuwatilia maananani kabisa. Lakini kwa huyu nikajikuta nikisimamisha gari na kumuangalia. Alitumia kama nusu saa hivi kufukua jalala huku na huko kama akitafuta kitu bila mafanikio.
Nikashuka ktk gari na kumfuata alipo, "Mwanangu ni nini unatafuta ktk jalala?" niliamua kumuuliza. "Baba ni siku ya pili hii sijatia kitu mdomoni njaa inaniuma sana wenzangu wamekua wakinishauri twende tukaibe lakini mimi sina ujasiri huo, hivyo siku ya pili nazunguka huku na huku kutafuta chakula lakini nakosa hakuna anaejali maisha gani haya?"
Moyo wangu ukawa kama umechomwa na kitu chenye ncha kali kusikia yale aliyoniambia!! Hapo hapo ikabidi nimchukue nikaenda kumnunulia chakula mgahawa wa jirani! Baada ya kula na kushiba akanishukuru na kuniambia " Baba Mwenyezi Mungu akubariki sana, naishi maisha ya tabu mno tokea mama yangu afariki. Hapa nilipo nina cancer" akafunua tshirt yake kunionesha, eneo lake la tumbo karibu na kitovu lilikuwa limeathiriwa vibaya na cancer. Akaendelea....
Mama yangu baada ya kufariki baba yangu aliamua kuoa mke mwingine, kusema kweli yule mama aliyeolewa na baba ni shetani!! Si mtu wa kawaida kabisa. Niliishi kwa mateso makubwa na yule mama wa kambo, kila nilipokuwa nikimueleza baba kuwa mama mdogo alikuwa akinitesa alikuwa haniamini hata kidogo, nilivumilia hivyo hivyo kwa tabu nyingi sana.
Kuna siku nikiwa jikon naosha vyombo mama yangu wa kambo alitembelewa na rafiki yake wa kiume. Katika maongezi yao nilisikia wakishauriana kuhusu kumuua baba na kujimilikisha mali zake zote, niliingiwa na wasiwasi mkubwa sana!! Nilisubiri baba arudi nimweleze hilo jambo. Aliporudi nilimueleza kila kitu nilichosikia. Maajabu baba alinipiga nusura ya kuniua akinituhumu kuwa simpendi mama yangu wa kambo. Kufikia hapa mtoto aliinama na kulia kwa uchungu. Nikachukua nafasi ya kumbembeleza.
"Laiti baba angalitia maanani maneno yangu angalikuwa hai mpaka leo"
Alinichapa baba, alinipiga kipigo cha mwizi mpaka nikavunjika kiganja cha mkono. Ni mpaka nilivokimbia na kutorokea mtaani. Na habari ya kwanza niliyoipata ni kuwa baba yangu amefariki.! Nikajua tu ni yule shetani ameshatenda ushetani wake. Nililia sana na ninalia mpaka kesho.
Yule mama aliuza kila kitu, ni kwamba baba alimrithisha kila kitu yule mama katika hati zake mbalimbali. Baba alikuwa na nyumba nne moja Mbezi Beach, kawe, Kigamboni na Msasani. Pia alikuwa anayo Insurance company iliyokuwa ikiitwa Junior Insurance Company Ltd Pale Posta, alikuwa na Super Market pale Nakumat, Pugu mall na kule shoppers plaza. Vyote vilienda kwa yule shetani.
Nikiwa sina sehemu ya kuishi tena, ndugu zangu wote wako Kigoma huko hakuna ambaye nina mawasiliano nae hata mmoja. Baba natamani Mungu anichukue hata leo. Ninaimani nitaenda kuiona mbingu, sitauona Moto wa milele kwa kuwa sijawahi tenda jambo la kumuudhi Mungu! Mimi siibi, mimi situkani wala sijihusishi na makundi ya wenzangu ya Panya Road.
Dah niliishiwa pozi. Nikajiambia kuwa kweli dunia haiko sawa. Ninaendesha gari zuri, ninaishi pazuri, ninayo kazi nzuri inayonipa mshahara mzuri, nakula chakula kizuri mpaka nakiacha, kumbe upande wa pili kuna watu wasio na hatia, malaika wa Mungu wakiteseka hivi? Nikitokwa na machozi mtu mzima.
Hapo hapo nikapiga magoti na kumshukuru mwenyezi Mungu, kwa kila jema analolifanya ktk maisha yangu, nikamuomba Mungu anisaidie niache tabia ya kulalamika na kutoridhika, watu pale mgahawan walinishangaa ila sikujali, nililia na Mungu wangu!!
Nilimchukua yule mtoto na kwenda nae Taasisi ya Cancer Ocean road kwa matibabu zaidi. Nipo nae mpaka leo hii akiendelea na matibabu hapa hospitalini, hali yake sio nzuri kwa kweli, he is serious sick!. Nitakuwa nae siku zote.
Kama Junior atakufa nitakufa pamoja nae
Nawatakieni kheri.
No comments:
Post a Comment