Wednesday, February 3, 2016

Repost.

Repost.http://safinamiutamu.blogspot.com/http://safinamiutamu.blogspot.com/
Wanauliza uko wapi wosia wa mama kwa bintie anaeolewa? Huu hapa!
Binti yangu, hivi sasa wewe ni mke wa mtu na karibuni utakuwa mama pia. Mungu amenibariki nishuhudie jinsi nilivyokufunza kupika na kufanya shughuli nyingine za nyumbani.
Nilikufundisha jinsi ya kuheshimu mume, na kutokuwa na hasira zisizo na msingi. Lakini kama utafanya vinginevyo, hutakuwa binti yangu niliyekuzaa bali mwanamke mwenzangu.
Binti yangu, unamuona mumeo? Ni gentlemen haswa! Ila usichukulie faida ya yeye kuwa gentlemen kumletea mizengwe. Usilete ujinga dhidi yake. Mwanangu unaona hili kovu kwenye paji langu la uso? Baba yako ndio alinips hili kovu.
Alinivumilia muda mwingi sana, ila siku moja from nowhere nilimuudhi tena, najua halikuwa lengo lake ila hasira zilimfika hapa akanipiga mara moja na kunumiza.
Mamii, Wanaume wanachukia pale unapomwambia "HUWEZI". Anajua anaweza akafanya zaidi ya hapo lakini anafanya hivyo kukulinda asikuumize. Binti yangu pale kutakapokuwepo na kutouelewana, jaribu kunywa maji, huwezi ukaongea huku maji yapo mdomoni.
Sasa una familia mbili. Una bahati sana mamii, Vumilia na heshimu familia yako kama ulivyokua ukifanya hapa. Jifunze kuwakarimu watoto wa majirani zako, na karibuni watoto wako wataizunguka meza yenu kwa upendo mkila pamoja chakula kwa furaha.
Unaliona lile hotpot langu kubwa? Nililinunua wakati bado sina hata mtoto mmoja, kabla ya kuwazaa ninyi. Lakini mara kadhaa nilipika chakula na kulijaza na kula pamoja na watoto wasio na pa kula.
Jifunze kuwa mkarimu, wakarimu wageni walau hata kwa maji ya kunywa. Usinyanyapae wageni, usidharau ndugu wa mumeo bali walete kwa pamoja. Jifunze ku appreciate jitihada ndogo zinazofanyika na karibuni watajifunza mengi kutoka kwako na watakupenda.
Leo umevaa shela la harusi, na unaonekana ni mzuri haswa lakini kuna gauni jingine utalivaa tena kwa miezi tisa! Gauni la ujauzito. Nami nililivaa pia.
Pale kutakapokuwa na kutokuelewana, usirudi hapa nyumbani. Msuluhishe wenyewe huko huko na jenga...

No comments:

Post a Comment

PESA YAIMBA WIMBO