MUHIMU:
Hakikisha unakuwa wa Muhimu pale ulipo, kama ni kwenye ndoa yako, mkeo afike aseme hakika hakuna mume bora au mme aseme wewe ni mke bora zaidi ya wote. Kama hata ukichelewa nyumbani huulizwi ulikuwa wapi? ujue huna umuhimu, mfano Kuna familia nyingine Baba akiondoka nyumba inakuwa na amani, ila akirudi watoto wanatamani kuhama nyumba.

Ikiwa ni kazini, fanya kwa Bidii na kwa Ubunifu hadi kama haupo kazini wakupigie simu maana kuna kitu hakipo sawa na wewe ndiye Unayefaa kukiweka sawa. Mfano kuna mwingine hata asipokuwepo kazini wiki hakuna anayemkumbuka, ujue wewe ni mzigo hapo kazini. Huu ni mfano mdogo Mungu Aliyemuumba wa vyote na mwenye Hekima zote akujalie Maarifa Ujuzi na Ubunifu katika Maisha yako, Ukayafanye yale yaliyowashinda wengine hata kama huna Elimu ya kiwango cha juu, AMEN (Mtume na Nabii Josephat E. Mwingira)

No comments:
Post a Comment