Wednesday, February 3, 2016

Baada ya malalamiko ya wabunge wa upinzani juu ya wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge, Spika wa Bunge, Job Ndugai, anatarajia kuzipangua kamati hizo.Taarifa ambazo zimepatikana mjini hapa jana, licha ya kuwapo kwa baadhi ya wajumbe walioomba kuhamishwa kwenye kamati walizopangiwa awali, kumekuwapo na mazungumzo kati ya Kambi ya Upinzani Bungeni na kiti ofisi ya Spika juu ya suala hilo.Inaelezwa kati ya wajumbe watakaohamishwa kutoka kwenye kamati zao za awali ni Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe analiyekuwa kwenye Kamati ya Maendeleo ya Jamii na sasa atapelekwa ya Hesabu za Serikali (PAC).Naye Mbatia aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Miundombinu, sasa atapelekwa kwenye Kamati ya Bajeti aliyokuwa akitumikia kwenye Bunge la 10. “Mbali na kambi ya upinzani bungeni, kulikuwa pia na shinikizo la mataifa ya nje ambayo yanataka hizi kamati za kuangalia serikali ziongozwe na upinzani, jambo ambalo Spika pia alikuwa anataka lakini kwa sababu fulanifulani ikawa kama ambavyo tuliona kamati zimepangwa awa,” kilisema chanzo kimoja cha habari kilichotaka kutotajwa jina lake.

No comments:

Post a Comment

PESA YAIMBA WIMBO