Thursday, November 19, 2015

TUSIMAME TASNIA ISIMAME

TUSIMAME TASNIA ISIMAME
Naifahamike wazi kuwa Tasnia ya filamu inakufa, na
hatuwezi kuendelea kulalamika kuwa tasnia ya filamu inakufa huku kila mmoja akiweka bawa lake pembeni, hatuwezi kukaa chini na kulia tu kwani machozi hayajawahi kuzima moto unaounguza nyumba bali walioacha kulia ndio huzima moto.
Si kama Watanzania hawawezi kutengeneza Filamu kubwa za Kimataifa ila Tuna matatizo sugu yanayotafuna Tasnia miaka na Miaka
Ikiwemo matatizo ya soko, elimu ya Sanaa, uwekezaji katika tasnia, sera ya fialamu, sheria na kanuni na mengineyo mengi ambayo yapo nje ya uwezo wa Msanii lakini siku zote tumekuwa tukilalamika tu na kufarijiana bila kuchukua hatua halafu vipindi vya kampeni wanasiasa wanatugawa kwa manufaa yao na kutuahidi ahadi zisizotekelezeka.
Hivi tujiulize wadau wa filamu, toka tuanze kugombana wenyewe kwa wenyewe au baadhi kujiona bora kuliko wengine tumeongeza thamani ya tasnia ya filamu kwa kiwango gani?.
Ikiwa inafahamika Secta ya Sanaa imeajiri kiwango kikubwa cha watanzania ila bado serikali imefumbia macho, Basi nini Kifanyike?
Tukutane Morogoro 27/11/2015 katika kongamano la kitaifa la wadau wa filamu kujadili mustakabali wa tasnia...
Tujadiliane, Tukubaliane na Tusimamie makubaliano yetu. Baada ya kongamano, tutazunguka nchi nzima kukusanya saini za wadau wa filamu kwa ajili ya kushinikiza utekelezaji wa maazimio yetu hata kama haupo Moro tutajitahidi kukufwata popote Ulipo.
Kwa watakaokuwa tayari kushiriki wapige simu au kutuma ujumbe kuthibitisha kwa:
Myovela
0715 578 730
Zagamba
0654 070 055
Mkindi
0716144134
Octa
0715444661
Ngabwe
0784646676
Pia unaweza ukaweka namba kwa ajili ya kukuunga whatsapp hii ni kwa wale wenye hiyo application na kwa wasio kuwa nao watumie sms za kawaida
SHARE KWA WINGI ILI WAHUSIKA WAPATE UJUMBE

No comments:

Post a Comment

PESA YAIMBA WIMBO