Serikali ya Swaziland, Imepiga marufuku wachawi kuruka zaidi ya umbali wa mita 150. atakaye kiuka amri hii iliyotolewa na mamlaka ya anga, atapigwa faini ya randi R500,000 (35,487) zaidi ya mil 80 za Kitanzania. Mara nyingi wachawi wa Swaziland wamekua wakiruka Usawa wa Helcopter kitu ambacho kinachanganya Mamlaka ya anga.

Kitendo hiki wachawi wamekilalamikia wakisema kwamba ni uonevu. wanahoji kwanini iwe sasa? Je walishawahi gonga Boeing?

Wakati huo huo Waganga wa kienyeji wa Romania wameangukiwa na rungu la kulipa kodi kubwa ili kuchangia bajeti ya Serikali kitendo ambacho Mkuu wa Sangoma hao amelalamikia kwamba ni Uonevu na kaahidi kuiroga Serikali isahau kuwalipisha Kodi hata ikikumbuka imsahau yeye tu. Baadhi ya Wachawi wameshukuru kitendo cha kulipishwa kodi kwani wanaamini sasa kazi yao imetambulika rasmi.

=====================Swaziland has launched a crackdown on high-flying witches after banning them from hovering above 150metres.