Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa mchezo wa soka hususani barani Ulaya hakika jina laMike Dean sio jina geni masikioni mwako, Mike Dean ni refa ambaye alianza kazi ya kuchezesha mechi za mpira wa miguu toka mwaka 1985, Mike Dean huwa anafahamika kwa mapokeo yake baada ya goli kufungwa.
Mike Dean amewahi kutuhumiwa kushangilia magoli yakifungwa wakati yeye akichezesha mechi, iliwahi kutokea February na April mwaka 2012, Dean amekuwa akituhumiwa kushangilia magoli kwa lugha za ishara, sasa bado haijaeleweka kama huwa anashangilia kwa mapenzi au hutokea tu anafanya hivyo. November 4 naomba nikusogezee video zaMike Dean akishangilia baada ya magoli kufungwa wakati yeye akiwa refa wa mchezo.
No comments:
Post a Comment