Saturday, November 21, 2015

Dk. Tulia Ackson AONJA YAMOTO BUNGENI.

Dk. Tulia Ackson AONJA YAMOTO BUNGENI.
Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, amekalia kiti hicho kwa kuanza kuonja 'joto la jiwe' baada ya kushindwa kujibu swali lililomtaka aeleze muda gani aliojiunga na Chama cha Mapinzuduzi (CCM) huku akikumbana na zomea zomea kali kutoka kwa wabunge wa vyama vya upinzani.
Mtafatuku huo uliibuka ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana, wakati Dk. Tulia alipokuwa akijinadi kwa wabunge kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi wa Naibu Spika.
Nafasi hiyo ilikuwa ikiwaniwa pia na Mbunge wa Kaliua (Cuf), Magdalena Sakaya, ambaye kura 101 alizopigiwa hazikutosha kumfanya akalie kiti hicho dhidi ya Dk. Tulia aliyepata kura 250.
Hata hivyo, swali lilosababisha bunge hilo kuvurugika lilitoka kwa Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko (Chadema), ambaye alimtaka Dk. Tulia atoe ufafanuzi muda wa uanachama wake ndani ya chama hicho, na kama mtumishi wa serikali ataje siku aliyotangaza kuachia ngazi na kujiunga na CCM kwani sheria na kanuni za utumishi wa serikali inamzuia kujiunga na chama chochote cha siasa.spot.com/http://safinamiutamu.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

PESA YAIMBA WIMBO