Dada alikuwa airport akisubiri connetion ya ndege yake, wakatangaziwa ni 2 hrs waiting time.
Akaamua kununua gazeti na box Dogo la biscuits, akatafuta sehemu akakaa
kusoma gazeti kusubiri muda ufike wa kuingia kwenye ndege, alipokaa
pembeni yake kulikuwa na kaka nae anasoma gazeti akisubiri ndege. Dada
alishangaa alipokuwa akitoa biscuit kwenye box aliloliweka pembeni yule
kaka nae anachukua moja anakula, akamwangalia kwa hasira, kaka akawa
anatabasamu.
Dada akakasirika akataka
kumtolea maneno machafu akajizuia. Ukawa mchezo kila dada akichomoa
biscuit moja yule kaka nae anachukua moja. Ikaendelea hadi ikabakia
biscuit moja. Yule kaka akawahi kuichukua akaimega nusu akampa yule
dada, ...dada kwa ghadhabu akanyanyuka akamtukana sana yule kaka na
maneno ya kumdhalilisha kwanini anavamia vitu vya watu asinunue vyake!!
Kaka alikaa kimya bila kumjibu yule dada.
Mara wakatangaziwa muda wa kuingia kwenye ndege, yule dada akaingia
akimuacha kaka nae akisubiri ndege yake. Alipokaa kwenye siti yake
akafungua mkoba aweke simu yake, mara alishtuka kuona box lake la
biscuits zima wala halijafunguliwa, kumbe alikuwa anakula biscuits za
yule kaka. Akajutia sana akatokwa na machoz jinsi alivyomdhalilisha yule
kaka, na muda wa kurudi kuomba msamaha haupo tena kwani milango ya
ndege ilishafungwa na kuanza kuondoka.
"Muda wa kuomba msamaha kwa uliyemkosea upo usisubiri milango ifungwe"...
Kiburi ni sifa ya Shetani
Nawatakia siku njema nyooote!
GOnga LIKE PAGE na kisha SHARE na marafiki
vichekesho zaidi soma na BONGO PUBLISHER BOFYA HAPA


No comments:
Post a Comment