Maombolezo
Mlango 1
1 Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa, Huo uliokuwa
umejaa watu! Jinsi alivyokuwa kama mjane, Yeye aliyekuwa mkuu kati ya
mataifa! Binti mfalme kati ya majimbo, Jinsi alivyoshikwa shokoa!
2
Hulia sana wakati wa usiku, Na machozi yake yapo mashavuni; Miongoni
mwa wote waliompenda Hakuna hata mmoja amfarijiye; Rafiki zake wote
wamemtenda hila, Wamekuwa adui zake.
No comments:
Post a Comment